CCM Shinyanga Kunafuka moshi mweusi!!

CCM Shinyanga Kunafuka moshi mweusi!!

Manjagata

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2012
Posts
16,526
Reaction score
18,608
Sasa hivi chama kinapumlia mashine, hii ni baada ya ujio wa Pombe aina ya "Mapuya" Joseph Magufuli hapa Shinyanga na kujifanya hamnazo na kujikuta akiropoka mbele ya kadamnasi kwamba kuna watu mchana ni CCM na usiku ukiingia wanahamia UKAWA. Katika mkutano wake huo alimtaja Gasper Kileo (GAKI) kama msaliti. Siku hiyo almanusura mkutano uingie dosari. Sasa kwa vile GAKI amekuwa mfadhili wa ccm kwa muda mrefu, kitendo cha kutajwa hadharani kama msaliti kimemwumiza sana pamoja na wapambe wake, hivyo wamekuwa na roho ya kinyongo kwa mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga town kupitia ccm.

Mtifuano huo ndani ya ccm ni faraja kubwa sana kwa UKAWA na ni ishara wazi kabisa kwamba jimbo hili ni la UKAWA, ije mvua, lije jua!! Masele hana chake na hii inachagizwa na mtifuano uliopo ndani ya ccm na umahiri wa kujieleza wa mgombea wa UKAWA kupitia CHADEMA (Patrobas "Mzimu wa Shelembi" "Sauti ya Zege" Katambi). Naomba hili jimbo liorodheshwe kwenye majimbo ambayo UKAWA tayari wameshajihakikishia ushindi.

Asante YESU kwa kuyafanya haya yatimie!!!
 
Unaongea kitu ambacho huna uhakika.Upinzani shinyanga hakuna kabisa.na CCM watachukua majimbo yote.wadanganye wasio ijua shinyanga
 
Mkuu Shinyanga namshauri mgombea wa CCM aache tu kuangaika ingawaje nasikia tarehe23/24/10 hawatalala watakuwa wanagawa fedha kuanzia elfu hansini na kuendelea hasa vijijini wanaamini watu wa vijijini wanakumbuka fadhira.
 
hauijui Shinyanga wewe gamba kaa kimya
Umeona mkuu eeh? Huyu jamaa mjinga sana anajidai kuijua Shinyanga kuliko sisi tuliopo hapa mjini! Kwa ufupi Masele angeacha tu akaenda kuitumia hiyo hela kwenye mambo mengine!! Hapa mjini hapati kitu, hiyo habari ya kura 1 mwaka huu haiwezekani kabisa!!
 
Unaongea kitu ambacho huna uhakika.Upinzani shinyanga hakuna kabisa.na CCM watachukua majimbo yote.wadanganye wasio ijua shinyanga
Wewe Suleiman ngosha a.k.a Suleiman Nchambi mwaka huu unachezea kichapo huko huko Kishapu kwa Mpendazoe hufurukuti!!
 
Umeona mkuu eeh? Huyu jamaa mjinga sana anajidai kuijua Shinyanga kuliko sisi tuliopo hapa mjini! Kwa ufupi Masele angeacha tu akaenda kuitumia hiyo hela kwenye mambo mengine!! Hapa mjini hapati kitu, hiyo habari ya kura 1 mwaka huu haiwezekani kabisa!!

Wewe ndiyo huijui shinyanga .na mnaanzisha thread kuudanganya umma .Masele anachukua jimbo kama kawaida na nchambi ndiyo hana mpinzani kabisa kishapu.
 
Umeona mkuu eeh? Huyu jamaa mjinga sana anajidai kuijua Shinyanga kuliko sisi tuliopo hapa mjini! Kwa ufupi Masele angeacha tu akaenda kuitumia hiyo hela kwenye mambo mengine!! Hapa mjini hapati kitu, hiyo habari ya kura 1 mwaka huu haiwezekani kabisa!!

Nani atampa ubunge mgombea wa chadema ambaye hana hata choo shinyanga ,anafanya kampeni akitokea guest house
 
Wewe Suleiman ngosha a.k.a Suleiman Nchambi mwaka huu unachezea kichapo huko huko Kishapu kwa Mpendazoe hufurukuti!!

Mpendazoe,
Yule aliyechemsha Segerea??
Mpendazoe ambaye analilia michango ya kampeni fb?
Au huyu ni Mpendazoe mpya?
 
Sasa hivi chama kinapumlia mashine, hii ni baada ya ujio wa Pombe aina ya "Mapuya" Joseph Magufuli hapa Shinyanga na kujifanya hamnazo na kujikuta akiropoka mbele ya kadamnasi kwamba kuna watu mchana ni CCM na usiku ukiingia wanahamia UKAWA. Katika mkutano wake huo alimtaja Gasper Kileo (GAKI) kama msaliti. Siku hiyo almanusura mkutano uingie dosari. Sasa kwa vile GAKI amekuwa mfadhili wa ccm kwa muda mrefu, kitendo cha kutajwa hadharani kama msaliti kimemwumiza sana pamoja na wapambe wake, hivyo wamekuwa na roho ya kinyongo kwa mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga town kupitia ccm.

Mtifuano huo ndani ya ccm ni faraja kubwa sana kwa UKAWA na ni ishara wazi kabisa kwamba jimbo hili ni la UKAWA, ije mvua, lije jua!! Masele hana chake na hii inachagizwa na mtifuano uliopo ndani ya ccm na umahiri wa kujieleza wa mgombea wa UKAWA kupitia CHADEMA (Patrobas "Mzimu wa Shelembi" "Sauti ya Zege" Katambi). Naomba hili jimbo liorodheshwe kwenye majimbo ambayo UKAWA tayari wameshajihakikishia ushindi.

Asante YESU kwa kuyafanya haya yatimie!!!

Siyo mafarakano, ni mzimu wa dhuluma, kumteka na kuchania form za nec ni dhambi isiyokuwa na msamaha mbele za mbingu. Uchaguzi uliopita ulikuwa bao la mkono, kitengo maalum kilimpitisha kwa kumbeba kwa mbeleko.
 
Chaguzi za mitaa tulipata neema ya kuhongwa elfu 10@, ubunge mjiandae na laki 1@.
 
Back
Top Bottom