CCM Sasa Ni Wakati wa Accomodations & Reconciliations!!


Unaweza kuongea uongeavyo kwa sababu umekuwa mvivu wa kusoma. Soma katiba ya zanzibar na ufikirie kama "inazungumzika" ukishapata jibu ufikirie na huo uharo uliouandika hapo juu. Kuna mtu aliwahi kusema "ukiona mtu anaishabikia ccm ujue ana kasoro fulani hivi" ninawiwa kuunga mkono usemi huo.
 
Kama tungebahatika kuwa na viongoi wenye hekima, kulikuwa na uwezekano wa kupata katiba ya Watanzania wote iliyo nzuri lakini bahati mbaya tunao hawa tulio nao. Kuanzia sheria yenyewe ya uundwaji wa katiba mpya ilifanyika kiujanjaujanja kama si kiujinga ujinga.

Mapungufu makubwa ya mchakato huu yalianzia kwenye sheria yenyewe ambapo iliruhusu uundwaji wa katiba kufanywa na wanasiasa. Mwenyekiti wa chama ndiye aliyechagua wajumbe wa tume badala ya wajumbe kuteuliwa na taasisi za wananchi. Wabunge walioshinda kwa rushwa, wizi wa kura na njama mbalimbali ndiyo limekuwa kundi kubwa la kuunda katiba ya kulinda utu na kujenga maadili. Rais aliyeshinda kwa kutumia hela za EPA ndiye anakuwa kiongozi wa kutoa mwongozo wa bunge la katiba katika kuunda katiba inayosisitiza uadilifu! Tume ya uchaguzi inayolalamikiwa kuwa ni tume ya kusimamia maslahi ya CCM ndiyo itakayosimamia upigaji kura za kupitisha katiba mpya, n.k.

Lazima uwe mbumbumbu kupindukia kuamini kuwa katiba mpya itakuwa na vipengere vya kuzuia uovu unaopendwa na kukumbatiwa na CCM. Na kama kuna mtu yeyote anayeamini hivyo nitamshangaa sana.

Watanzania waliache jambo hili lipite, katiba ya wananchi itaandikwa na wananchi wenyewe walio waadilifu siyo wabunge walioshinda uchaguzi kwa rushwa. Hilo litawezekana pale tu tutakapoupata uongozi wenye maono, dhamira na nia njema, unaojali na kuheshimu maamuzi ya wananchi, uongozi wenye uadilifu siyo uliopatikana kwa hela za EPA au hela nyingine yoyote iliyo chafu.

Watanzania tupiganie kuuondoa utawala hodhi na wa rushwa, na kujenga utawala mpya ulio safi. Tutakapopata uongozi wa namna hiyo, ndipo wananchi watapewa haki na uhuru wa kuandaa katiba inayowafaa. Tusipotezee muda mwingi kuzungumzia huu mchakato kiini macho uliopewa jina la katiba mpya. Katiba inayotengenezwa sasa ina uwezekano wa kuwa hovyo kuliko katiba yoyote tuliyowahi kuwa nayo.

Katiba zilizotangulia hazikushirikisha wananchi lakini viongozi walioziandaa wakati huo walikuwa wazalendo na wenye nia njema siyo kama manyang'au wa sasa.

 
Elimu ndogo tu, 'Aliesababisha matatizo hawezi kuyatatua matatio aliyoyasababisha', maana hata uwezo wa kuyatambua ni matatizo, hana. Ndiyo maana CCM inaendelea kushikilia ilichoamini siku zote, wenye akili wanavyouona mwungano si kama wanavyouona CCM.

 
WILLIAM,

whats your opinion on the referendum for Zanzibar Independence?

- Jamani samahani sana nilikuwa nimesafiri na sikuwa na access ya mtandao was too busy, ok mkuu sana naomba uelewe kichwa cha hii mada hayo unayoyauliza hapa sio mahali pake fungua thread yake mkuu!!

Le Mutuz
 

- Kama nimekuelewa wewe una akili sana kuliko hii mada sasaiweje tena uje uijibu mkuu unajivua nguo kuwa una kasoro flani, maana ukiona mtu anajibu anayoyaita hayana maana basi ujue hana maana au nimekosea kaka?


Le Mutuz
 
Ukikuta wajinga wanagombania mzigo wa mavi basi bora uendelee na safari yako la sivyo na wewe watakupaka kinyesi

- Ok this is great thinker, basi I am out of here mpaka zitokee hoja nzito U know!!

Le Mutuz
 
Nina swali kws muanzisha uzi huu. Hivi 2010 wakati Zanzibar wanaandika katiba inayosema kwamba wao ni nchi, wakaenda mbali zaidi na kuweka kifungu kinachozuia sheria isitumike Zanzibar hadi ijadiliwe Baraza la wawakilishi, Raís alikuwa wapi na ccm yake, leo ndio aje hapa kusema wanaweza kutatua matatizo ya muungano?? Isitoshe ameshindwa kuitetea na kuilinda katiba ya nchi. Miaka 50 ya muungano kuna kero nyingi kuliko faida, kubalini mmeshindwa kuongoza nchi wapeni wengine tuone.
 
Nina swali kws muanzisha uzi huu. Hivi 2010 wakati Zanzibar wanaandika katiba inayosema kwamba wao ni nchi, wakaenda mbali zaidi na kuweka kifungu kinachozuia sheria isitumike Zanzibar hadi ijadiliwe Baraza la wawakilishi, Raís alikuwa wapi na ccm yake, leo ndio aje hapa kusema wanaweza kutatua matatizo ya muungano?? Isitoshe ameshindwa kuitetea na kuilinda katiba ya nchi. Miaka 50 ya muungano kuna kero nyingi kuliko faida, kubalini mmeshindwa kuongoza nchi wapeni wengine tuone.
 

- Hizi ni changamoto tu za Muungano zinahitaji kurekebishwa ila sio za ajabu mpaka kudai kuvunja Muungano!!

Le Mutuz
 
nawaomba wale wabunge wanaotaka kura ya wazi wakae upande wao na wale wanaotaka kura ya siri wakae upande wao na wakati wa kupiga kura wale wabunge wa wazi wapige kwa uwazi tuone wamechagua nini na wale wa siri wapige kwa siri wanavyotaka. alafu na sisi wananchi tupewe fursa hiyohiyo anaetaka kupiga kwa wazi apige ili kila mtu ajue amechagua nini na wale wa siri wapige kwa siri. ila mimi kama gogo la shamba naweka wazi kwamba,mke wangu,mtoto wangu au ndugu yangu yeyote anaenitegemea atakaepiga kura kinyume na ninavyotaka mimi atafute mtu mwingine wa kumtegemea. maana ndivyo ccm wanavyotaka.huo ndio msimamo wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…