CCM sasa kama mnara wa Babel

CCM sasa kama mnara wa Babel

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Posts
654
Reaction score
184
Na Padre Baptiste Mapunda (M.afr)
frmapunda91@gmail.com

Sasa ni dhahiri kwamba mwelekeo wan chi yetu umetufikisha mahali pabaya. Haya tumeyasema, tumeyaandika, wengine tumeyahubiri, lakini serikali yetu tukufu ya CCM haisikiii. Mara nyingi kwa watu kama hao imeona ni “maadui nambari wani”. Ni kitu cha kusikitisha kwa taifa kama hili ambalo ni changa lakini lenye kubarikiwa na mwenyezi Mungu.

Waswahili husema “ kwenye miti hakuna wajenzi.” Siasa za nchi ya Tanzania zilianza vyema na Baba yetu wa Taifa Mwalimu JK Nyerere ambaye anaweza kufananishwa kama “Musa” aliyewatoa Waisraeli utumwani. Kazi ya kuleta ukuombozi ni kazi ngumu sana kwa kiongozi na waongozwa, kwani inahitaji ubunifu, upendo, uzalendo, heshima, utu na uvumilifu mkubwa sana.



Mwalimu JK Nyerere alijenga taifa lenye umoja, heshima, undugu, usawa, upendo, amani na haki chini ya siasa za “Ujamaa na kujitegemea” kama dira yake ikaimiarishwa na Azimio la Arusha. Mwalimu alijitahidi kufuta utemi na kuwaunganisha Watanzania kwa kuongea lugha moja ya kindugu. Hata hivi baada ya Mwalimu kufa, viongozi waliofuata walianza kuachana na misingi mizuri aliyoiasisi.

Leo nchi yetu imegawanyika vipande vipande chini ya serikali ya CCM. CCM ya Nyerere ilikuwa na Umoja, dira, sera nzuri za taifa, ilikuwa na upendo. CCM ya Nyerere ilipendeza na kupendwa na Watanzania karibu wote. Lakini CCM ya leo inayounda serikali ya Tanzania imegeuka na kuwa kama ‘mnara wa Babel’ (Mwanzo 11:19). Kwa nini naifananisha CCM ya leo na mnara huo? Ni kwa sababu ya hali halisi ya siasa katika nchi yetu.

Waisraeli walipofika katika nchi ya Shinar waliamua kufyatua tofali na kujijengea mji na mnara ili kuichungulia mbingu kwa majivuno ya kujiona wao sasa ni sawa na Mungu. Wakasema ngoja tujitengenezee jina kwaajili yetu. Lakini Mungu aliposhuka toka mbinguni alipoona jinsi walivyojaa majivuno, kiburi, madharau, ulevi wa madaraka akawasambaratisha kwa kuwachanganya wasisikilizane tena.(Mwanzo 11:1-9). Na huo ndiyo ukawa mwisho wao.

CCM ya sasa imekuwa kama Mnara wa Babel, hakuna umoja, upendo, amnai, kuamini, heshima, dira, sera za kujali wanyonge, kuwatumikia wananchi. Ndani ya CCM ya kuna kejeli, vitisho, kiburi na ubabe; sasa kwa nini tuifananishe na Mnara wa Babel? Askofo Mkuu Zakaria Kakobe alishatoa utabiri wake kama huo huo, kwamba CCm itasambaratika, na je nini kinaendelea kutokea hadi leo hii na hasa ukitazama kilichojiri katika Bunge la katiba huko Dodoma?

CCM inazidi kujikaanga kwa kupanga kila aina ya mizengwe, hila, fitina, unyanyasaji kwa raia na wapinzani hata kwa kutumia jeshi la polisi na vyombo vya usalama wa taifa. Je, hii si alama ya kusambaratisha kama Mnara wa Babel? Mungu wetu ni Mungu wa haki, mtu mwenye fitina, na chuki, hatafika mbali maandiko yanasema. Kuendelea kujidanganya kwamba CCM inaendelea kupendwa na inakubali na Watanzania wengi ni kuonyesha upofu wa hali ya juu na ulevi wa madaraka. Matokeo yake ni kugeuka dikiteta ambayo ni alama wazi ya kushindwa kuendesha nchi kwa kufuata sheria, kanuni na katiba ya nchi yetu.

Bahati mbaya kuna wanaCCM na viongozi wa serikali ambao kwa makosa ya fikra zao, kiburi na utamu wa madaraka bado wanajidanganya na kuamini kuwa CCM itadumu milele. Hawa pamoja na mashabiki wao wapenda madaraka na mafisadi wamejiaminisha katika upotofu wao kuwa Chama hiki cha Mapinduzi kitatawala milele, kitadumu milele na kitaendelea kuwa kama kilivyo sasa milele milele na milelel, Amina! Hawa ni wale wanaotakiwa kuombewa kwani wana “pepo la ulevi wa madaraka” ambao ni ugonjwa.

Nikiendelea na unabii niseme tu kwamba CCM ni tunda la fikra na kazi ya binadamu; ni chombo kilichoundwa na wanadamu, kinaongozwa na binadamu kwa hiyo CCM ni chombo kinachoweza kuharibika, kuvunjika, na mwishowe kinaweza kufa. Vyama vingi vikongwe barani Afrika kama Kenya (KANU), Malawi, Zambia (UNIP) na kadhalika. Busara za kibinadamu zinatuambia kuwa ‘kila kitu kina mwanzo na mwisho’. Na hivi CCM lazima itafika mwisho kama siyo leo ni kesho, na kama siyo kesho, keshokutwa hii ni kawaida.

Na watu wengine wanapokaribia kufa huwa wanahangaika na kutapatapa sana wakijaribu kujiuliza kwa nini mimi kutafuta mchawi wao ni nani? Leo hii CCM inahangaika sana kutafuta mchawi wake ni nani, na hivi kupoteza muda mwingi kushughulika na wapinzani jinsi ya kuwadhibiti badala ya kujenga sera za kuwakwamua Watanzania kutoka katika lindi la umaskini. Mchawi wa CCM ni CCM wenyewe lazima ifike mahali wajitafiti nchi hii inadai mabadiliko je wapo tayari kuyaongoza mabadiliko hayo kwa uslama na umakini?

Saikolojia ya magonjwa ya akili inatufundisha kwamba dawa pekee ya kupona magonjwa hayo yawe ya akili, ulevi wa madwa na pombe ni kujikubali kwamba una tatizo la sivyo utaendelea kusteseka. Hivyo ninaposikia mtu anasema kwamba hakuna ufisadi ndani ya CCM ninamshangaa. Nikimsikia mwanasiasa anasema “CCM ni safi” naendelea kumshangaa zaidi mwenzetu anaongelea CCM gani ya Nyerere au hii ya leo?

Pia ninapowasikia wanapropaganda wa CCM wamekazana kuiitetea CCM kuwa ni chama safi na kina “mafisadi wanne” tu ninafumba macho yangu na kujiuliza “hivi ni kweli” au ni porojo? Au hii ni alama ya kukata tama na alama wazi ya kugeuka mnara wa Babel na ulevi wa madaraka. Matukio ya ajabu tunayoyasikia sasa na kuyashuhudia hivi sasa ndani ya CCM ni alama wazi kwamba chama hiki kikongwe barani Afrika hakika kiko matatani na hakuna mtu wa kuiokoa. CCM haiokoleki kwa sababu imegeuka na kuwa kama mnara wa Babel.
 
Nakubaliana na wewe. Zaidi nazani CCM itapasuka kutokana na migongano ya kimasilai na kushindwa kubebana katika ufisadi maana nauhakika hakuna usawa katika kufaidika na ufisadi CCM
 
Hakuwezi kuwa na usawa kama wanawapa ubunge mpaka std VII na wenye MSc wanawaburuza wao Ndioooo!
 
Kinana akienda kwenye mikutano anasema 'serikali haiwajibiki'. Sasa sijui yeye yuko chama gani. Chama tawala ndo serikali nikimaanisha rais, mawaziri, wakuu wa mikoa na wa wilaya na wakuu wengine ni wa chama tawala, CCM. Kwa hiyo anaeleza watu kuwa CCM haiwajibiki. Na watu wanaomsikia sijui kama wanaelewa hilo. Ushabiki bila kufikiri ni ujinga. Namaanisha, wanaohudhuria mikutano yake ni ma-ze-ze-ta.
 
Jamani hata mimi huyu Kinana na Nape wananishanhaza sana. Wameamua kuwaona.watu ni mazuzu. Nilishasema ni kwanini hakai vikao na hawa watu anaowaona hawawajibi na kuzungumza nao kwa kuwa ni wa chama chake? Anapotangazia umma kuwa mawaziri walioteuliwa na chama chake ni mizigo anakuwa na maana gani? Je, alijisikiaje alipowaahidi wananchi mawaziri mizigo wangeondolewa madarakani lakini hadi leo wako madarakani? Hakuna uongozi wa pamoja. Ni kweli CCM ni kama Babeli. Kinana na Nape wamedhirisha hili.
 
Jana yule kijana aliyempiga Babu Warioba alidai kuwa wapinzani wameambiwa waanzishe SACCOS kwani wamezidi kwenda kuomba fedha kwa wahisani. Mona hakuwaeleza kuwa chama chake kinakwiba fedha za walipa kodi?
 
Back
Top Bottom