Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,552
- Thread starter
-
- #21
Hoja nimeipenda, nitairudia kuchangia lakini naomba kwanza nianze na huu wimbo. Mbona mmebadilisha maneno yake? Kwa kumbukumbu yangu huu wimbo ni wa kichaga, niliwasikia sana wakiuimba enzi tuko Moshi (wakati huo CCM ilikuwa na miaka miwili tu!). Enzi hizo watumishi wa serikali walikuwa wanalazimika kujiunga na mgambo ili wapate cheo kwenye CCM, tulikuwa tunawasikia wakiimba huu wimbo pale uwanja wa shule ya Msingi Muungano ambayo ilikuwa nyuma ya ofisi za RDD wa Moshi:
CCM kyaambalama kocheenyi,
CCM kyaambalama kocheenyi,
CCM kyaambalama kocheenyi CCM eeeh,
Kocheenyi CCM kyaambalama kocheenyi!
Sikuwahi kusumbuka kutaka kujua maana yake wakati huo, lakini kwa kuwa mmenikumbusha naomba wachaga walioko kwenye forum hii wanipe tafsiri yake.
Fukuto la fukuta, moshi wafoka, mapovu yanamwagika, CCM imefika njia panda! Ama isuke au inyoe!
Hili vurugu la Richmond, likizingirwa na BOT EPA, BOT CIS, BOT Minara, Rada, Kiwira, Buzwagi na moto kutoka Upinzani, unafanya mambo kadhaa tujiandee kutokea.
Kutokana na kuwepo makundi haya makubwa na utata unaotambaa angani hasa baada ya Lowassa kuangushwa na minong'ono kuwa naye Lowassa ana ushahidi wa kujikosha, linalobakia kwetu watazamaji ni kupima upepo na kuomba dua wapigane na wagawanyike ili tujue nani ni kwa manufaa ya Taifa na nani ni mnyonyaji.
- Wabunge ambao si mtandao, wenye uchungu wa kweli wa CCM, kuendelea kusulubisha viongozi wao na Serikali yao iwe wazi. Hawa wabunge, mwokozi wao na nguzo yao ni Wastaafu Malecela, Kawawa, Mwinyi, Salim na Msuya. Huku wako hawa walioshupalia RDC;-Mwakyembe, Kilango-Malecela, Seleli, Kimaro, n.k.
- Team Mkapa; huku ni wale wajanja wa Che-Nkapa ambao bado wanatibu majeruhi ya mchakato wa kugombea Urais 2005 na kunyang'anywa tonge la Hatamu za Chama. Hapa kuna Mang'ula, Ngwilizi, Kigoda, Kinana, Warioba na Ruhinda. Katika kundi hili, pia wapo wale waliotajirika na mradi wa Ujasirimali Ikulu; Yona, Mramba, Mgonja, Mkono n.k.
- Mtandao; Kundi hili lina majeruhi wengi kutokana na kuvunjwa kwa baraza la mwazirina mwegemeo wa kashfa za ufisadi kuwa kwenye shingo zao. Kundi hili, limegawanyika katika sura mbili;
- Team Kikwete ambayo wamebakia Makamba, Chiligati, Membe, Migiro, Karume
- Team Rostwassa(Rostam/Lowassa); Karamagi, Msabaha, Nchimbi, Apson, Meghji, Kamala, Diallo, Chenge,
- Wasiofungamana lakini wana nguvu na ni tishio; Pinda, Mwandosya, Sumaye, Balali, Salmin, Magufuli, Msekwa na Sitta.
Nanukuu baadhi ya mambo ambayo yanaashiria kuwa huko CCM si salama, na hata kama wakitoka nje ya ukumbi wakiwa wamekumbatiana, tusiwaamini.
Rev kishoka...lazima uanzishe thread kila ukisoma gazeti linakuvutia? si lazima kila mtu aanzishe thread...hata hujui ipi muhim...take time kusoma walichoweka wenzako, then weka mchango na sources zako.
Pia Muhimu kuweka the whole story? au http link inatosha..mnajaza space bila mpango ktk JF.
Hivi ndivyo ilivyo JF , mbona munatutisha sisi Junior member , kwa nini mtu asitoe mawazo yake - la muhimu ni kuchangia hoja na sio kukandia thread za mwenzako.
Team Kikwete ambayo wamebakia Makamba, Chiligati, Membe, Migiro, Karume
Team Rostwassa(Rostam/Lowassa); Karamagi, Msabaha, Nchimbi, Apson, Meghji, Kamala, Diallo, Chenge,
Wasiofungamana lakini wana nguvu na ni tishio; Pinda, Mwandosya, Sumaye, Balali, Salmin, Magufuli, Msekwa na Sitta.
naomba munieleweshe wana JF wana brass ndio nani thanks
Mkuu wangu Rev,
Maneno mazito hayo, Sitta ni mtandao haswa, ila tamaa za urais ndio zinamponza, ccm is ok maana sasa the brass ndio wenye power wakiitumia idara, muungwana ndiye aliyeko matatani maana akifanya mchezo the brass wanaweza kumuweka mkuchika 2010, otherwise, ya kwako ni great analysis!