CCM nzima inashindana na Lissu?

CCM nzima inashindana na Lissu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,169
Reaction score
48,451
Kwa jinsi inavyoonekana ni kama vile chama chote cha Mapinduzi kinafanya kila kitu si kwa maslahi ya Tanzania bali ili kuonesha kwamba Tundu Lissu hayuko sahihi kwa hoja anazozitetea.

Nakumbuka tangu enzi bunge linaendeshwa na Anne Makinda sheria nyingi za hovyo zilipitishwa kwa kuonesha "serikali" iko sahihi na Lissu kakosea.

Lissu inawezekana kachukua nafasi ya Dr. Slaa wa "enzi zile" ambapo alipingwa na CCM kwa kila jambo alilolifanya.

Hata Leo Lissu yuko kitandani Hospitalini Nairobi anaumwa, naona harakati zinazofanywa kushindana naye. Hata yale aliyoyasimamia leo yanapotoshwa kwamba aliyapinga.

Lissu inawezakana watu wengine wanaona ni "mropokaji" lakini CCM ndiyo wanaoijua nguvu yake. Kila mwaka akigombea kwenye jimbo lake CCM huweka nguvu ya ziada na mkazo usio wa kawaida ingawa siku ya mwisho anayeibuka mshindi ni Lissu.

Nguvu ya CCM ni watu kukaa kimya, lakini ni chama dhaifu sana linapokuja suala la watu kuikosoa hadharani. Kuna wakati walitumia kuita watu kuwa si watanzania ili kuwatia hofu, sasa wamekuja na silaha nyingine kuwaita watu wasaliti na si wazalendo.

CCM nzima kuanzia kamati Kuu yake mpaka kwa balozi wao wa mtaani kwetu na kwenu, wako bize kuipaka matope haiba ya Lissu na kutaka kumfanya ni adui wa watu na maendeleo ya taifa.

Ninachojifunza CCM ni chama kilichokufa bali uwepo wake unategemea uhai wa kuazima toka kwenye vyombo vya dola. CCM wajue wanafanya kazi ya kuendesha serikali yetu kwa niaba ya watanzania wote na si kwa faida ya chama chao.
 
umesema kweli sasa hivi wamehamisha maovu ya serikali za ccm kuanzia mkapa kikwete na magufuli mabegani kwa Lissu huyo ndio kiboko yao yaani amewafanya wawe kwenye defensive yaani huu mjadala uliendelea ili kuprove kitu kwa lissu sio kusaidia nchi ndio maana wameshindwa wamepewa vipipi vya kulambishwa wana share wakikubali
 
Froida huo ni mfano mmoja tu. Nakumbuka yeye na Mnyika walivyokesha kuhusu sheria mbali mbali zilizopitishwa kwa wingi wa kura na mbwembwe na wabunge wa CCM!
 
Wanamuogopa Lissu kupita maelezo.

Hata kipindi fulani nadhani 2010 wakati wa kampeni Kikwete akiwa jimboni kwa Lissu alisema "bora Dr Slaa awe rais kuliko Lissu kuwa mbunge" hii inadhihirisha ni jinsi gani wanamuogopa Lissu.
 
Hadharani wanajikaza kisabuni ili waonekane hawatishwi na Lissu, lakini wakiwa faraghani wanatetemeka kama yule mzee kwenye lile shairi la "karudi baba mmoja toka safari ya mbali".
 
umesema kweli ila hawatakuelewa,maana hawa ni wafu wanaotembea kwa msaada wa K47
 
Hadharani wanajikaza kisabuni ili waonekane hawatishwi na Lissu, lakini wakiwa faraghani wanatetemeka kama yule mzee kwenye lile shairi la "karudi baba mmoja toka safari ya mbali".
yaani baada yakuona maamuzi ya leo wamechemsha sasa wanamuattack Lissu wakati wenyewe walipokuwa wanakula raha yeye alilala migodini na watanzania akiwatetea
 
yaani baada yakuona maamuzi ya leo wamechemsha sasa wanamuattack Lissu wakati wenyewe walipokuwa wanakula raha yeye alilala migodini na watanzania akiwatetea
Wanaacha maudhui ya anachokisimamia wanajadili jinsi anavyokisema anachokisimamia!!
 
Back
Top Bottom