kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,252
- 16,171
Kuna msemo unasema CCM ina wenyewe, hao wenyewe ni akina nani?
Kila kikundi/chama kina waanzilishi wake ambao ndio huwa Na sauti Na heshima kubwa mbele au nyuma ya pazia. Sauti Na heshima hizo huwa zinarithishwa kwenye kizazi cha waanzilishi hao. Chadema, NCCR, ACT, Chauma, NRA, TLP, nk vinafahamika waanzilishi wake Na wanayo sauti Na heshima kubwa kwenye taasisi hizo. Waanzilishi wa TAA iliyozaa TANU iliyozaa CCM na CCM yenyewe ni akina nani? wapo? watoto na wajukuu wao wapo? Wana sauti na heshima kwenye CCM?
Nilidhani kuwa CCM ni mali ya Mwl Nyerere, Kawawa, Kingunge, nk lakini siioni familia za Mwl Nyerere, kingunge, Kawawa, Rupia au nani wakiwa nyuma au mbele kwenye CCM.
Nyerere alisemaga kuwa CCM sio baba wala mama yake, angeweza kuachana nacho akimaanisha kuwa CCM INA wenyewe ambao sio yeye, kingunge aliikimbia CCM, na akina Mzee Makamba, Kinana, Nape, Polepole, Bashiru, malecela, Kolimba, na wengine wengi ambaao walionekana kuwa labda ndiyo baadhi ya wenye CCM nao kuna wakati walikutana na alichokutana nacho mtema kuni ndani ya CCM kuonyesha kuwa wenye ccm, wenye TANU na ASP na wenye TAA wapo lakini wamefichwa kwa makusudi au bahati mbaya kusikojulikana pamoja na familia zao.
Wenye CCM hawaonekani, hawana sauti wala heshima tena ndani ya ccm. CCM imekuwa dude lisilokuwa na mwenyewe linalotumika tu kuingiza watu Ikulu baaasi, likishafika Ikulu linageuka kuwa mmiliki wa CCM kwa 100% na kuwa tishio hata kwa waliokuwa wakidhani kuwa ni wenye CCM kindakindaki. Kundi litamnyoa bila maji yeyote mwenye mawazo mbadala na maslahi yao.
Linaweza kubadilisha chochote kwenye katiba ya CCM na ile ya nchi. Wengine woote kula yenu itategemea utashi na huruma zao hasa kwa vile litawahitaji baadhi yenu wakati wa chchaguzi tena.
Wanaweza kubadilisha katiba na sheria kuruhusu masilahi yao yashamiri na ikiwezekana wabaki madarakani milele. Utawqsikia kwa kupitia wanufaika wakisema "utake usitake tutakuongezea muda"
Wenye TAA, TANU na baadsae CCM na ASP wako wapi? Wanapata nini?