CCM ni mwanzo wa mwisho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ni mwanzo wa mwisho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAUMZA, Apr 18, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Tunaambiwa kuwa CCM imevua gamba. Nadhani huu unaweza kuwa ni mwanzo wa mwisho wa zama za CCM. Kwa nini ninasema hivi, nitaeleza baadae. Mawazo yangu yananituma kuwa mwisho na kiama cha CCm kinawadia/kimewadia. Jenga picha ikiwa Edward Lowassa na timu yake katika uongozi wa CCM na wafuasi wao nchi nzima wakiamua kuhamia CDM. Tukumbuke kuwa katika siasa hakuna adui wa kudumu au rafiki wa kudumu. Sitashangaa iwapo EL na wenzake wakakimbilia CDM au chama chochote, iwe NCCR, CUF, TLP etc.
  Inachokifanya CCM ni mauti kwao. Sidhani kama sekretariet hii mpya kama imeweza kurudisha imani ya wananchi kwa CCM. Sidhani!!! Je, Mukama ana mvuto zaidi ya Slaa waCDM? Je Nape ana mvuto zaidi ya vijana wa CDM akina Zitto na Lema? Haya yote ni mambo ya kujiuliza.
  Ushauri wangu ni huu, CCM(sekretariet) waache siasa za personalities na assassination. Zitawaumiza na pindi wakianguka wasahau kuinuka tena milele na milele. CCM wakumbuke kuwa kazi kubwa ya kwanza inayofanywa na chama chochote cha siasa pindi kinaposhika dola katika nchi zetu za dunia ya tatu ni kukinyong'onyeza chama kilichokuwa madarakani kabla.Wajiulize, ipo wapi KANU ya Kenya. Ipo wapi UNIP ya Zambia na ipo wapi MCP ya Malawi. Ninamhurumia JK. CCM ni nzito ameshindwa kuibeba na taifa ni zito zaidi. Ameelemewa. Kila kona, mara maandamano ya CDM, katiba mpya, maisha magumu, umeme na kila tatizo unalolijua wewe hapa nchini. JK sasa amechanganyikiwa hasa

  Hitimisho: Salama ya CCM ni ipi? (rhetoric question)!!! Ni kumuomba Mungu EL na kundi lake ndani ya chama na wafuasi wao wasiasi chama na kuingia CDM au chama kingine chochote kile. CCM, SAFARI IMEWADIA. JIANDAENI KUFUNGASHA VIRAGO
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Wameanzisha mkakti mbovu na wakati mbaya wangesoma alama za nyakati badala ya kukurupuka wakumbuke wamebeba dhamana ya nchi na ni jukumu lao kuhakikisha nchi inabaki salama
   
Loading...