Tunapoizungumzia CCM ni kumaanisha mkutano mkuu wa CCM ambao ndio kikao cha juu zaidi cha kupitisha maamuzi,,,kikao hiki wajumbe wake wengi sio sehemu ya serikali...hata hivyo mara nyingi kama sio mara zote maamuzi ya wajumbe hawa hutegemea zaidi kupisha yale yaliyopitishwa na halmashauri kuu ya CCM ambayo wajumbe wake wengi ni sehemu ya serikali...
Kwa kumalizia tu ni kwamba CCM na serikali ni sawa na familia nyumani ambayo baba na mama ndio halmashauri kuu na mkutano mkuu ni pale kikao kikijumuisha na watoto.