Elections 2010 CCM nao wameanza kuzoa mizoga

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Kuna habari kuwa wakati mgombea urais kwa tiketi ya CCM Jakaya Kikwete akiwa Mbalizi mkoani Mbeya alivuna wanachama wapya wapatao 400 wengi wao wakiwa wanachama wa Chadema akiwemo aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Mkoa wa Mbeya ndugu Ipyana Seme.

Habari zingine zinasema rais alidanganywa kwa kuonyeshwa kadi mpya feki kwa vile tayari bwana Ipyana na wenzake walishafukuzwa Chadema.

08_10_9ha1yf.jpg


Swali langu ni kwa nini CCM akiwemo katibu wake mkuu Makamba walikuwa wakiwaita mizoga wanaCCM waliokuwa wakihamia vyama vya upinzani wakati huo. Na ni kipi kilichowafanya sasa CCM kuikubali mizoga iliyokwisha temwa na wapinzani.

Nauliza hivyo kwa sababu kuna watu wengi tu wakiwemo wanaJF walikuwa wakiwaita majina ya ajabu ajabu watu waliokuwa wanatoka CCM kwenda upinzani kwa sababu mbalimbali, sijui leo watatuambia nini kwa hiki kitendo cha CCM. Je ni halali kwa CCM kupokea mizoga na si halali kwa upinzani kufanya hivyo. Tujadili.
 
Makamba ni sawa na gunia tupu, sawa na puto lenye hewa za kueleaelea, ubabe wa dhamana, lakini uongozi wake hauna nguvu za hoja bali ni za ubabe," alisema Shibuda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom