Ni nadra sana kwa chama chama cha mapinduzi kufanya mkutano mkubwa bila ya kuwashirikisha wasanii wa bongo fleva, au taarab nk. Nimekuwa najiuliza hivi bila hao wasanii hamtaweza kuvuta umati mkubwa wa watu? Mbona vyama vingine vinaweza kuvuta watu bila ya wasanii? Tumeshuhudia kwenye kampeni za Raisi kikwete 2010 akizunguka na wasanii wengi sana ktk kampeni zake,
tena huwatumia wasanii ambaoo wana mvuto kwa wakati huo!
Leo tumeshuhudia msanii anaependwa kwa sasa Diamond akiwa kwenye mkutano wao wa leo, mimi naamini wananchi wengi wamekuja kumwona Diamond na wala si Rais!
Naamini ccm haina mvuto tena kwa watu ndiyo maana wanatumia wasanii,
Msanii kama Diamondi anamvuto sana kwa vijana ndo maana ccm wamemlipa ml 8 aende kwenye mkutano wao.
Je kama ni hivi mtaweza kupambana 2015?
Tumeshuhudia mikutano ya ccm wakitumia pesa nyingi kwa kuwapa watu vitenge, kofia, tsheti bila kusahau vyakula! Je ndo wananchi wanataka au mnawatongoza kwa ajili ya kura 2015?
Hakika wananchi wa Tanzania chukueni hatua.