CCM na UKAWA Walimwa Barua

CCM na UKAWA Walimwa Barua

Sipendi Ubepari

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2012
Posts
249
Reaction score
40
Gazeti la Tanzania Daima kupitia ITV Magazeti asubuhi hii limesomwa na kuoneshwa kicha cha habari kwamba "UKAWA na CCM walimwa barua". Huku Songea hatupati mapema magazeti hayo, hivyo mwenye nakala ya gazeti hilo atubandikie hapa tuone ni mamlaka ipi imetoa barua hiyo kwa ccm na UKAWA.
 
Songea ipo Kenya? Someni The Citizen.
 
Hilo gazeti LA Mbowe tunafungia vitumbua hatusomagi sisi huku kwetu
 
Gazeti la Tanzania Daima kupitia ITV Magazeti asubuhi hii limesomwa na kuoneshwa kicha cha habari kwamba "UKAWA na CCM walimwa barua". Huku Songea hatupati mapema magazeti hayo, hivyo mwenye nakala ya gazeti hilo atubandikie hapa tuone ni mamlaka ipi imetoa barua hiyo kwa ccm na UKAWA.
wametaja gazeti la udaku la tz daima!!!!!! hilo ni sawa na magazeti ya udaku yanayomilikiwa na shigongo kama vile uwazi,ijumaa na kiu..take care mkuu.
 
Hilo gazeti LA Mbowe tunafungia vitumbua hatusomagi sisi huku kwetu
linaandika habari za mapenzi ya jinsia moja yanayofanywa usiku pale bilicanas club ya mbowe
 
Gazeti la Tanzania Daima kupitia ITV Magazeti asubuhi hii limesomwa na kuoneshwa kicha cha habari kwamba "UKAWA na CCM walimwa barua". Huku Songea hatupati mapema magazeti hayo, hivyo mwenye nakala ya gazeti hilo atubandikie hapa tuone ni mamlaka ipi imetoa barua hiyo kwa ccm na UKAWA.

Sijaiona Hiyo Habari Ndugu, Ila Pitia Hapa www.freemedia.co.tz Usome Vizuri Mwenyewe Kama Kweli Ipo.
 
Gazeti la Tanzania Daima kupitia ITV Magazeti asubuhi hii limesomwa na kuoneshwa kicha cha habari kwamba "UKAWA na CCM walimwa barua". Huku Songea hatupati mapema magazeti hayo, hivyo mwenye nakala ya gazeti hilo atubandikie hapa tuone ni mamlaka ipi imetoa barua hiyo kwa ccm na UKAWA.

Kwa sababu inaonekana kuna tatizo la Mtandao, kwa faida ya swali lako naomba kuiweka stori hii ilivyo:

CCM, Ukawa walimwa barua

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vitatu vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi vimetumiwa ujumbe mzito wa barua kutoka kwa Wanataaluma wa Kikristo Tanzania (CPT) ya kuvitaka viridhiane kwa maslahi ya taifa ili wananchi wapate Katiba mpya, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.
CPT ambayo ipo chini ya Kanisa Katoliki, wamesema kuwa wamechukua hatua hiyo kwa kuwa mchakato huo umeliacha taifa katika mpasuko ulioletwa na hoja za vyama vya siasa ndani ya Bunge Maalum la Katiba.

Kwa mujibu wa barua hiyo ambayo gazeti hili limenasa nakala yake ya Mei 13, mwaka huu, yenye kumb.CPT/L/-C/14/12 kwenda kwa makatibu wakuu wa CCM na NCCR Mageuzi, Chadema na CUF vinavyounda Ukawa, inasomeka kuwa; "tuonavyo sisi kuna haja kubwa ya maridhiano ili kuwezesha mchakato wa kuendelea hadi kuwapatia watanzania Katiba mpya.

Vile vile sababu kubwa ya malumbano ndani ya Bunge Maalum la katiba ambayo hanaya tija kwa nchi yetu na watu wake ni upotoshaji wa makusudi wa sheria inayoongoza mchakato. Watu wamechoka na mambo yanayoendelea nchini. Wazo la katiba mpya linachukuliwa kama nyenzo; watu wameiona kama njia au nyenzo ya kufikia upatikanaji wa mabadiliko wanayoyatamani".
Kwa mujibu wa CPT, maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba hadharani na kwa njia ya wazi yaliwaaamsha watu kuhusu dhima yao katika utawala wa nchi na uundwaji wa katiba yake.
"Watu walitoa maoni yao wakiwa huru na kwa namna, na katika njia na majukwaa huru, walitegemea yabainishwe katika taarifa na rasimu ya tume ya Warioba, na ni kweli taarifa na rasimu ya tume vimezingatia kwa kiwango kikubwa maoni yaliyotolewa na wananchi na kukusanywa na tume hiyo,"alisema.
Barua hiyo iliongeza kuwa hadi sasa taarifa na rasimu ya tume ya Warioba iko njia panda, imekwama na imekwamishwa na wanasiasa na mtuhumiwa mkuu ni chama tawala ambacho kwa makusudi hakitaki kuipa rasimu rasmi ya katiba hadhi yake stahiki kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 kama ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 2013 kifungu cha 25 (2).

"Rasimu ya tume ya Warioba inaweza kuboreshwa na Bunge Maalumu la Katiba kwa masharti ya kufafanuliwa, kupanuliwa upeo au wigo wake, kuyaimarisha bila kutoka nje ya misingi yake, tunu na nguzo zake za kimsingi zinazotokana na kuaswa kwa kiwango kikubwa na maoni ya wananchi kwa madhumuni ya kutunga katiba mpya,"anasomeka barua hiyo.

CPT imeonya wajumbe wa Bunge la Katiba kuacha kufanya siasa za kivyama kwenye badala yake waikubali rasimu ya tume ya Warioba kama inavyotakiwa na sheria kama msingi halali wa kutafuta muafaka wa kitaifa kwani rasimu hiyo iliwasilishwa na Rais mwenyewe kwa taarifa yake Januari 22 mwka huu.
Hata hivyo, CPT imemtaka Rais Kikwete kuomba radhi kwa kuondoa kwenye misingi na njia yake rasmi iliyowekwa kisheria. Pia wanataaluma hao walionya kuwa kama wanayoasa hayawezi kupatikana kwa hiari, itabidi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Bunge Maalumu la Katiba kuomba mahakama yenye mamlaka kutofa tafsiri sahihi ya vifungu husika kisheria na kikanuni kuhusu mwenendo wa Bunge hilo.
Source – Tanzania Daima
 
Hilo gazeti LA Mbowe tunafungia vitumbua hatusomagi sisi huku kwetu

Huko kwenu mnasoma Uhuru na Mzalendo tuu ili kupata matangazo yale ya waganga wa kienyeji (chini ya udhamini wa Kingunge). Tumekuelewa vizuri, yale magazeti yenye habari za kina na uchunguzi hamuwezi kusoma maana yako juu ya uwezo wenu wa kutafakari na kuelewa.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Hilo gazeti LA Mbowe tunafungia vitumbua hatusomagi sisi huku kwetu

acha kujifariji,kwa hapa Mwanza magazeti yenye soko ni Tanzania Daima,Mwananchi,Raia mwema na Mwana........ Tu,mengine yaliyobaki ni ya kufungia vitumbua tu!
 
wametaja gazeti la udaku la tz daima!!!!!! hilo ni sawa na magazeti ya udaku yanayomilikiwa na shigongo kama vile uwazi,ijumaa na kiu..take care mkuu.

Mkuu magazeti ya shigongo mnayaita ya udaku kwa kuwa yanfichua uovu unaotendeka katika jamii na kumbuka mwandishi ni kioo cha jamii ambapo jamii hujiangalia na kujisahihisha pale ilipopotoka. Uonevu wa kijinsia na mauaji yanaripotiwa na UWAZI kwenu ni udaku. Mmomonyoko wa maadili (ukahaba,ushoga, ufuska) hasa wa watu waliopewa dhamana kubwa katika jamii kwenu ni udaku. Wakati mwingine ni vema tukajifunza kuchuja taarifa tunazopewa sio kuwa kwa vile kiongozi fulani au tabaka fulani linayaita magazeti ya udaku basi nasi tufuate mkumbo. pili tukumbuke kila jamii inahitaji taarifa zinazogusa maisha yake ya kila siku hivi mlalahoi wa manzese,kigilagila nk anaguswa vipi na tenda za kuchimba gesi kwenye gazeti la Mwananchi au Citzen wakati haujui mlo wake wa jioni utakuwa nini.
 
Gazeti la Tanzania Daima kupitia ITV Magazeti asubuhi hii limesomwa na kuoneshwa kicha cha habari kwamba "UKAWA na CCM walimwa barua". Huku Songea hatupati mapema magazeti hayo, hivyo mwenye nakala ya gazeti hilo atubandikie hapa tuone ni mamlaka ipi imetoa barua hiyo kwa ccm na UKAWA.

Subirin wakati komba anaenda msituni atawapitishia magazeti hapo
 
Back
Top Bottom