VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Wakati mwingine CCM inajidhalilisha. Hata kama ni ubunifu,huu si vutizi. Ni kukipaka matope chama kutokana na tafsiri zinazochomoza tokea hapo. Nyuma kidogo,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba alikuwa akizunguka nchi nzima kwenye mikutano ya chama na kijana Mussa Tesha aliyedaiwa kumwagiwa tindikali Igunga.
Ikadaiwa na kutangazwa mikutanoni na Mwigulu kuwa Tesha wa Igunga alimwagiwa tindikali na CHADEMA katika harakati zao za ugaidi. Tesha akazungushwa na kuoneshwa kama mfano wa ugaidi wa CHADEMA. Ilipoonekana mbinu hiyo imegonga mwamba au haina mvuto, ikaachwa.Sifahamu Tesha wa Igunga sasa yuko wapi na anafanya nini.Na alifaidikaje na kutembezwa kila kona ya nchi na Mwigulu.
Sasa CCM imeibuka na kali ya muongo huu. Inatumia wanyama aina ya fisi katika mikutano yake hasa ya Kanda ya Kati-Dodoma na Singida. Sijaweza kupata mantk ya kuwatumia fisi. Kama ni kujaza watu wanaokuja kushangaa,basi chama hakiko sawa. Inabidi kama chama tawala tujaze watu kwenye mikutano yetu bila matumizi ya fisi kwa mema tunayoendelea kuyafanya kwa watanzania.
Kama ni kuongeza idadi ya wahudhuriaji kwa kuwaleta na fisi,hiyo ni aibu kubwa kubwa kwa viongozi na chama kwa ujumla. Hatupaswi kufanya hivyo. Ndiyo maana nasema tumetoka tindikali ya Tesha wa Igunga hadi kutumia fisi. Tuache mara mbinu za kukitweza na kukisawajisha chama!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam