CCM na sura ya utawala kikoloni

Binomial

Member
Jun 23, 2015
48
12
Wakoloni waafrika ni hatari zaidi ya wakoloni weupe.

Martin Luther Jr. alishawahi kuzungumza juu ya wazungu kuiita Afrika, The dark continent. Juzi juzi Donald Trump amezungumza juu ya watawala wengi wa kiafrika kuuibia umma kisha kwenda kuwekeza mataifa ya magharibi. Ujinga ulioje!

Wakati nikisoma juu ya sifa za utawala wa kikoloni napata shida kuutofautisha na wa sasa labda tofauti pekee ni kwamba wale walikuwa wazungu na hawa watanzania wenzetu hebu tazama;

Matumizi ya vyombo vya dola. Kipindi cha ukoloni wa kizungu vyombo hivyo vilitumika kuwatisha na kuwaadhibu wale waliojaribu kwenda kinyume au kupinga utawala. Hali ndivyo ilivyo sasa wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi wanaadhibiwa kila uchao tena ndani ya bunge huku wengine wakidhalilishwa.

Sheria kandamizi. Wakoloni walitengeneza sheria ambazo zilimnyima mwafrika Uhuru. Vyombo vya habari vilivyojadili juu Uhuru wa mwafrika vilipigwa marufuku. Leo hali ni ileile, sheria za makosa ya mtandao na sheria za magazeti ni mfano halisi.

Uzuiaji mikusanyiko. Kipindi cha ukoloni ilizuiwa sana isipokuwa ile iliyounga mkono ukoloni. Hali ndivyo ilivyo sasa baada ya serikali kupiga marufuku mikutano ya kisiasa.
Mwisho niwaambie kwamba ni jukumu letu kuhakikisha Tanzania nchi bora kwa vizazi vyetu.
 
Back
Top Bottom