CCM na STYLE ya Kulia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na STYLE ya Kulia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Feb 13, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Diwani wa Kata ya Kisangura (CCM),
  Katika Tarafa ya Rogoro wilayani hapa, Joseph Muniko, amelazimika kumwaga machozi mbele ya mkutano wa kijiji cha Bisarara ili kukwepa adhabu dhidi yake kufuatia hatua yake ya kumzaba kibao kijana mmoja kwa `kosa` la kukamata kuku wawili kutokana na vijana wa diwani huyo kutoshiriki shughuli za maendeleo.

  Tukio hilo lilianza Februari 8, mwaka huu kijijini hapo baada ya kundi la vijana wanaolingana kwa umri, maarufu hapa kama `saiga` walipokamata kuku wawili wa diwani huyo kama faini kwa kitendo cha watoto wake kugoma kushiriki katika shughuli za maendeleo.

  Kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na kaimu katibu tarafa ya Rogoro, Masaga Magesa, kitendo hicho kilimuudhi diwani huyo aliyechaguliwa Oktoba 12, mwaka jana katika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha diwani aliyekuwepo, ambapo aliamua kuwafuatilia kuku wake hao ili kuwarejesha.

  Huku uamuzi wa kukamata kuku ama kulipa faini ya sh. elfu 10,000 kwa wanaokwepa kushiriki shughuli za maendeleo ukiwa ni wa kijiji, diwani huyo alifika na kuchuka kuku wake kwa nguvu huku akisema hayuko tayari kulipa kiasi hicho na wala kuku wake kuchukuliwa.

  Inadaiwa diwani huyo wakati anachukua kuku hao kibabe, vijana waliokuwa wamemkamata kuku wake waliamua kumtolea uvivu na kumwambia kuwa yeye ni kikwazo cha maendeleo, kauli iliyomuudhi zaidi na kumzaba kibao kijana mmoja wao kisha akaondoka na kuku wake, huku akitamba kuwakomesha.

  Imeelezwa kwamba kitendo hicho kiliwaudhi wananchi wengi ambao waliamua kwenda nyumbani kwa diwani huyo, wakachukua ng`ombe wawili zizini akiwemo maksai mmoja na kuwapeleka katika ofisi ya kijiji.

  Habari zimesema kwamba diwani huyo aliamua kuchukua sime na kufuata ng`ombe wake kibabe hali iliyopelekea wananchi kuogopa kutokana na jinsi wanavyomfahamu kwamba anaweza hata kuua, hatua iliyomwezesha kuondoka na ng`ombe wake wawili na kurudi nao nyumbani kwake.
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama ni style ya CCM, lakini wameongozana
  -Spika Sita
  -Mheshimiwa Pinda
  -Zombe
  -Bageni
  -Diwani wa Kata ya Kisangura (CCM), Joseph Muniko
  -.......
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  DU! kama na maagizo ya viongozi yangefuatwa kama hivi anavyofuatwa PM basi tungekuwa mbali. Lakini hiyo sasa ni suluhisho kwani Wabongo tunaogopa machozi.
   
 4. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Diwani katumia ubabe halafu baadaye akalia? Mbona hadithi yenyewe haieleweki, mwanzo inaanza na diwani kulia lakini mpaka mwisho yeye anaondoka na ng'ombe bila mtu kumwambia kitu...Sasa alilia baadaye?
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kufuatana na gazeti la nipashe .. stori inaendelea.......

  Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Edward Ole Lenga, aliitisha mkutano wa hadhara Jumatano wiki hii ambapo aliongozana na mkurugenzi mtendaji, polisi wawili na kaimu katibu tarafa kwa nia ya kumkamata diwani huyo kwa vitendo hivyo, hususan lile la kutisha wananchi kwa sime wakati akifuata ng\'ombe wake.

  Hata hivyo, mkuu wa wilaya, katika hatua ya kulinda heshima ya kiongozi huyo alibadili msimamo na kuitisha kikao cha viongozi pembeni kwa lengo la kumtaka Mniko aeleze ni sababu zipi zilizomfanya aamue kufanya hivyo.

  Habari zinasema kwamba diwani huyo alikiri kutenda makosa hayo huku akikana kuchukua sime.

  Hatua hiyo ya kukiri kwa mkuu wa wilaya haikuishia hapo kwa kuwa wananchi walikuwa wakimsubiri kumsulubu ambapo Mkuu wa Wilaya alipowaruhusu kujumuika kwenye mkutano wake walianika kila kitu huku wakikaribia `kummeza` Muniko.

  Habari zinasema diwani huyo alimwaga machozi huku akiomba msamaha kwa jamii na kwa viongozi wa wilaya kutokana na makosa aliyotenda.

  Alidai yuko tayari kulipa faini ya sh. 50,000 kwa kitendo cha kurejesha ng\'ombe kwa sime na sh. 20,000 kwa kurejesha kuku huku akimzaba kibao kijana mmoja wapo.
   
 6. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii kali...yaani ukimwaga chozi kesi zote zinafutwa? Hawa mahabusu wetu hawajashtukia hili dili nini?
   
 7. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hapa CCM wanajaribu tu kuiga alichofanya Hillary Clinton New Hampshire primary na kushinda..
   
 8. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  ...kuna Mkurugenzi wa halmashauri moja ya wilaya pia aliangua kilio kwenye mkutano baaada ya kubanwa atolee maelezo shilingi milioni 120 zilivyotumika.
  Hiyo naona ni stahili sasa!
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  zombe naye aliangua kilio mahakamani.
  Je? Mahakama itamfutia mashitaka anayokabiliana nayo !!
   
 10. m

  msabato masalia Senior Member

  #10
  Feb 15, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa nini hawa watu wasianzishe bendi kama lady jd.Wingi wa chozi.....................
   
Loading...