Gwaje
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 299
- 86
Miaka ya 1995 na 2000 wakati wa uchaguzi viongozi wa CCM na wagombea wao kupitia mikutano mbalimbali na hata TV ya taifa walikuwa na kampeni yenye mlengo mbaya kwa vyama pinzani kwa kupandikiza chuki ya udini. Enzi hizo chama kilichokuwa na nguvu zaidi za kiupinzani kama CUF kiliitwa jina la ngangali na kilihusishwa na uislamu na kampeni zilipigwa wakristo wasikichague kwa kuwa ni chama chenye udini ndani yake. CCM ilikuwa pia ikirusha picha za mauaji ya Rwanda na Burundi kama ishara au onyo kwa watanzania wasichague chama hicho. Pia miaka ya hivi karibuni hasa 2010 serikali na CCM ilipoona kumeibuka chama kingine cha siasa chenye nguvu za kutaka kuchukua nchi yaani CHADEMA, viongozi hao kwa TV ama mihadhara wakaanza tena kupanda mbegu za udini kwamba CDM ni chama cha udini na hasa ukristo. Bahati nzuri awamu hii mbegu hii imekubari kuota na sasa matunda yameanza kuonekana na hapa serikali na CCM inaibuka na kujifanya inashangaa suala hili la udini limetoka wapi? CCM imeanza kwa maana hii CCM inakataa kuwa ndio muasisi wa UDINI nchini