CCM na Serikali Mnajiangamiza wenyewe

CCM na Serikali Mnajiangamiza wenyewe

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,746
Nafikiri wana JF tumepitia kwa kina na kujadili pia juu ya sakata la Pembe za Ndovu naomba tulinganishe Kauli hii ya waziri Nchimbi na hali halisi ya matukio haya je vinashabihiana?

Dk Nchimbi ajibu mapigo

Akijibu tuhuma hizo, Waziri Nchimbi alisema: “Ukiona mtu anasimama na kuamua kusema kuwa hakuna kinachofanywa na wizara kuhusu masuala ya ujangili, ni wazi uelewa wake unakuwa na utata mkubwa.”
Alisema hoja zilizojengwa dhidi ya Kinana ni uongo mtupu... “Nimejaribu kufuatilia kwa makini alichokisema alikimaanisha, alikielewa, alikitafakari au aliandikiwa tu akaenda kusoma? Baada ya kutafakari kwa kina nikagundua hakuwa na nia mbaya, aliandikiwa tu na ameenda kusoma,” alisema Dk Nchimbi.
Alisema ukweli wa jambo hilo ni kwamba ipo tofauti ya majukumu ya kampuni za Wakala wa Meli na shughuli za kupakia mizigo bandarini huku akituhumu kambi ya upinzani kuwa inajua ukweli lakini imeamua kupotosha umma.
Dk Nchimbi ambaye alikuwa mchangiaji wa kwanza, alisema wakala hawezi kuwa mmiliki wa meli, bali anamwakilisha mwenye meli kwenye shughuli ndogondogo zinazofanyika inapofika nchi fulani kama kuhudumia watumishi wa meli, mahitaji muhimu na kufanya usafi.
“Lakini kuna watu wanaitwa ‘clearing and forwarding (Kupakua na kupeleka mizigo). Napenda kukwambia Mchungaji Msigwa kuwa kazi yao ni kupeleka na kutoa mizigo bandarini,” alisema Dk Nchimbi na kuongeza;
“Kule ndiko kuna utaratibu wa upekuzi, katika utaratibu wa upekuzi mtu wa ‘shipping agency’ (wakala wa meli) hahusiki, sina shaka hata kidogo Mchungaji Msigwa analijua hili ninalolisema, ila amelifumbia macho kwa makusudi kwa masilahi yasiyokubalika katika taifa.”
Alisema kumekuwa na uvumi ambao umekuwa ukifanywa kwa makusudi kuwa Kinana anahusika na meli iliyohusika kusafirisha pembe zile.
“Uvumi huu ni uzushi, meli iliyobeba mizigo ile inaitwa Delmas Nakadha, mmiliki wake anaitwa Bus Herman Ledley jambo hili Kambi ya Upinzani Bungeni inalijua, ila kwa masilahi yasiyokubalika katika taifa wameamua kupotosha Bunge lako,” alisema.
Alisema baada ya uchunguzi wa kutosha, wahusika walibainika na ikafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 3 na 4 ya mwaka 2009 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
“Hawa (anawataja) ndiyo waliopelekwa kortini, uchunguzi ulijidhihirisha kuwa ndiyo watuhumiwa wa jambo hili, Kambi ya Upinzani Bungeni inalijua,” alisema.

Oktoba 21, 2012
Maafisa wa forodha wa Hong Kong wamegundua karibia tani nne za pembe za ndovu haramu zilizofichwa katika bidhaa kutoka Kenya na Tanzania wiki hili, AFP iliripoti siku ya Jumamosi (tarehe 20 Oktoba 2012).
Idara ya forodha ya Hong Kong ilisema mzigo huo una thamani ya dola milioni 3.4 na ni pamoja na vipande 1,209 vya meno ya tembo na mapambo yaliyotengenezwa kwa pembe za ndovu yaliyofichwa katika maboksi yaliyoandikwa "plastic scrap" na "roscoco beans". Ilikuwa na uzito wa tani 3.81, na kuifanya kuwa ukamataji ulio mkubwa kabisa wa pembe huko Hong Kong hadi sasa.
Mamlaka za China zimewakamata watu saba kuhusiana na magendo hayo, ikiwa ni pamoja na mkaazi mmoja wa Hong Kong. Magendo ya pembe za ndovu huko Hong Kong yanachukua muda wa miaka saba jela na kulipa faini ya dola 258,000.
Biashara ya Kimataifa ya pembe za ndovu, isipokuwa mara chache sana, imezuiliwa tangu mwaka 1989 baada ya idadi ya tembo huko Afrika kushuka kutoka mamilioni katikati ya karne ya 20 hadi kama 600,000 mwishoni mwa miaka ya 1980. Hata hivyo mahitaji ya pembe za ndovu huko Asia na Mashariki ya Kati yameongeza biashara haramu.
Mapema mwezi huu mamlaka za Tanzania ziliomba haki ya kuuza pembe za ndovu zilizolimbikizwa ili kugharamia hatua za ulinzi wa tembo.
[h=2]Polisi wawakamata majangili wanne wa tembo jijini Dar es Salaam[/h]Oktoba 30, 2012
Polisi wa Tanzania waliwakamata wanaume wanne kuhusiana na kumiliki pembe za ndovu 214 jijini Dar es Salaam Jumamosi (tarehe 27 Oktoba 2012), Gazeti la The Guardian la Tanzania liliripoti.
Polisi walipata pembe za ndovu, zenye thamani ya shilingi bilioni 2.2 (dola milioni 1.4 ), kutoka katika nyumba waliyoikagua baada ya kupata fununu kutoka kwa wakaazi, alisema Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Suleiman Kova. Pia walikuta seti za televisheni zilizoibwa, kompyuta, mafriji, magodoro, mikrowevu na vitu vingine.
Washukiwa ni pamoja na Watanzania wawili na Wakenya wawili. Washukiwa watafikishwa mahakamani hivi karibuni, Kova alisema.
Ukamataji huu umekuja wiki mbili baada ya mamlaka za Tanzania kukanusha usafirishaji wa magendo wa pembe za ndovu tani 3.81 zilizokamatwa Hong Kong.

[h=2]Tanzania yakataa kujihusisha na pembe za ndovu zilizokamatwa[/h]Oktoba 22, 2012
Viongozi wa Tanzania wakataa kuhusika na tani 3.81 pembe za ndovu za magendo zilizokamatwa huko Hong Kong mwishoni mwa wiki, wakidai kuwa idadi kubwa kama hiyo ya pembe za ndovu haiwezekani kuwa zimetoka nchini kwao, gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti siku ya Jumatatu (tarehe 22 Oktoba 2012).

Pembe za ndovu zilizokamatwa katika operesheni dhidi ya biashara ya magendo huko Hong Kong zikioneshwa kwenye mkutano wa vyombo vya habari hapo tarehe 20 Oktoba.2012 [Na Dale de la Rey/AFP]
Viongozi wa Hong Kong walisema kuwa pembe hizo zilikuwa zimesafirishwa kutoka Kenya na Tanzania na zilikuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 3.4
"Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuwia uwindaji haramu wa tembo na wanyama wengine wa msituni," alisema Paul Sarakikya, afisa wa wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania. "Inaweza kutokea kwa kesi adimu sana, lakini kiwango kikubwa kama hicho cha pembe za ndovu haziwezi kuwa zimekusanywa kutoka nchini."
Sarakikya alisema kuwa wawindaji haramu wanaofanya kazi hiyo katika nchi zisizo bahari kama vile Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo au Mozambiki hutumia bandari ya Dar es Salaam kusafirisha bidhaa zao, na kuongeza kuwa bandari inapaswa kufanya upekuzi zaidi wa makontena yanayotoka nje ili kuzuwia biashara haramu ya pembe za ndovu.
Hivi karibuni Tanzania iliomba idhini kutoka kwa Makubaliano ya Kimataifa juu ya Biashara ya Kimataifa ya Wanyama Walio Hatarini ili kuuza baadhi ya lundiko la pembe zake za ndovu, zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 87.8 (dola milioni 55.

[h=2]Meno ya Tembo yenye thamani ya shilingi milioni 200 yapatikana huko Songea[/h]Februari 24, 2013
Maskauti wa vijiji na kitengo cha kuzuia ujangili cha Wizara ya Maliasili na Utalii walipata meno ya tembo yenye thamani ya shilingi milioni 200 (dola 123,000) katika Mbuga ya Wanyama ya Selous katika Mkoa wa Ruvuma, gazeti la The Guardian la Tanzania liliripoti Jumamosi (tarehe 23 Februari 2013).
Waangalizi wa wanyama pori, pamoja na msaada kutoka kwa Game Frontiers of Tanzania (GFT) na Jamii ya Eneo la Usimamizi wa Mbuga ya Mbaran'gandu, pia walikamata bunduki moja, alisema Bernard Lijaji, kaimu mkuu wa hifadhi ya kanda ya magharibi.
Kitengo cha kuzuia ujangili kimekuwa kikiendesha doria ya mara kwa mara katika mbuga tangu mwezi Januari kwa kutumia fedha kutoka GFT. Mzunguko wake utaendelea hadi operesheni ya uwindaji itakapofungwa mwezi Juni.
Mwaka jana Tanzania iliomba kibali kutoka kwa Makubaliano ya Kimataifa juu ya Biashara ya Kimataifa ya Wanyama Walio Hatarini kuuza shehena yake ya pembe za ndovu, maombi ambayo iliahirisha mwezi Januari ili kuboresha udhibiti wa ujangili na kuimarisha vizuizi vinavyohusu magendo ya pembe za ndovu.
Ripoti iliyowasilishwa bungeni mwaka 2012 ilikadiria kwamba tembo 30 wanauawa nchini Tanzania kila siku.
"Ujangili wa tembo ni wa kiwango kikubwa na unahitaji rasilimali za kutosha kupunguza kiwango cha tatizo," alisema naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu.

[h=2]Polisi Tanzania watoa zawadi kwa habari za ujangili[/h]Februari 27, 2013
Polisi wa Tanzania wameahidi "zawadi kubwa" kwa habari zitakazopelekea kukamatwa kwa watuhumiwa waliotelekeza gari yao na vipande 18 vya pembe za tembo zenye thamani ya shilingi milioni 29.4 (dola 18,000), gazeti la The Guardian la Tanzania liliripoti siku ya Jumatano (tarehe 27 Februari).
Habari zilipeleka kuikamata gari ya washukiwa hao siku ya Jumamosi jioni katika Mbuga ya Taifa ya Milima ya Udzungwa. Waliokuwemo kwenye gari walikimbia, na kuacha vipusa, alisema kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile.
Inaelekea vipusa hivyo vilichukuliwa kutoka maeneo ya Ifakara au Mahenge, ambako kiasi cha tembo tisa waliuliwa hivi karibuni, alisema mhifadhi mkuu wa Mbuga ya Taifa ya Milima ya Udzungwa Vitalis Turuka.

[h=2]
[/h]
[h=2]Polisi Tanzania yamkamata kijana akiwa na pembe 13 ya tembo[/h]Machi 29, 2013
Polisi ya Tanzania imemkamata mwanafunzi mmoja wa sekondari kwa tuhuma za kuwa na pembe 13 ya tembo katika eneo la Kimara katika wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti siku ya Ijumaa (tarehe 29 Machi 2013).
Christopher Julius, mwenye umri wa miaka 18, alikamatwa tarehe 22 Machi na alibakia chini ya ulinzi wa polisi, alisema Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Dar es Salaam Suleiman Kova.
"Kukamatwa huko kulitokana na taarifa kutoka kwa raia wema wanaofuata sheria ambao waliwaarifu polisi waliokuwa katika doria kwenye eneo ambalo mwanafunzi alikuwa na pembe ya tembo kwenye begi lake, lakini thamani ya vipande hivyo haikuweza kufahamika mara moja," Kova alisema.

My Take.
1. Naomba kuuliza tu majibu ya Nchimbi yalihusisha pia na habari hizi zilizoripotiwa na vyombo hivi vya habari? maana naona maelezo yake yanaishia 2009 wakati matukio makubwa yameripotiwa 2012 na ndiyo Meli za Kunana zilihusishwa.

2. Kwa nini Tanzania ilijitoa katika tuhuma juu ya Meno yaliyokamatwa Honkong kwamba serikali haihusiki wakati waliokamata wamesema yametoka Tanzania na Kenya.

3. Tuna hazina ya kutosha ya meno ya Tembo ambayo Serikali iliomba kupunguza kwa kuyauza, je kiasi kilivokuwa hapo awali bado idadi yake ipo hivyo hivyo?
 
Back
Top Bottom