makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,219
Wana JF,
Watanzania bado tunajiluliza nini hasa kimewapata hawa Viongozi wa CCM na Serikali yao? Kila kukicha tunashuhudia matusi, mipasho, kejeli za kijinga. Tumesikia matusi mpaka ya nguoni kwenye Bunge Maalumu la Katiba na sasa jambo lile lile linaendelea kwenye Bunge la Bajeti!
Inasikitisha sana kuona kwamba ndugu zetu wa Upinzani wanakuwa na hoja za msingi sana na za kujenga Taifa. Lakini kinachotokea ni Serikali kupitia Bunge na Serikali wanapinga hoja hizo kwa kejeli, mizaha,dharau na matusi. Hii ni aibu kwa Serikali ya CCM kufanya mizaha kwenye hoja za msingi.
Kwa watazamaji walioko nje ya Bunge kinachoonekana ni kuwa Wabunge wa CCM ndiyo wamegeuka kuwa Wabunge wa upinzani kwa kupinga kila hoja inayoibuliwa na Vyama vya upinzani. Tangu Bunge la Bajeti limeanza tumeona hoja za kina Mbowe, Tundu Lissu, Mnyika, Lema na Wabunge wa vyama vingine wakikejeliwa,kupuuzwa na kutukanwa kana kwamba wanayozungumza ni uzushi.
Hivi inakuwaje kwa mfano Mbunge au Waziri wa CCM anasimama na kumshutuma Mbunge wa Upinzani kuwa ni mchochezi na mwongo ilhali Mbunge huyo anaongea kwa data? Hivi ni nani mchochezi kati ya Mbunge wa CCM Bwana Komba aliyesema ataingia msituni kupigana kama mfumo wa Serikali 3 utakubalika? Nani mchochezi kati ya Lukuvi na Tundu Lissu? Lukuvi alienda Kanisani na kuchochea kuwa kama Serikali 3 zikikubaliwa basi Zanzibar itatawaliwa KIISLAMU kwa utawala wa SHARIA na kuwa WAKRISTO huko Zanzibar hawataruhusiwa kuabudu makanisani. Lakini pia akadai kuwa mfumo wa Serikali 3 ukiruhusiwa Jeshi litachukua Madaraka! Pamoja na kuropoka uchochezi huu Lukuvi anaonekana ni malaika mtakatifu, lakini Lissu anayehoji mambo ya msingi kuhusu Muungano ndiye anaonekana mchochezi na mwana wa Shetani!
Hivi ni vihoja na vichekesho vya karne kwa Watanzania!!! Watanzania wote wenye akili timamu hawakubaliani kabisa na ujinga huu wa Serikali ya CCM. Kama ni uchochezi basi CCM ndiyo wachochezi wa kwanza. Tumewasikia Katibu Mkuu wa CCM Bwana Kinena na Katibu mwenezi wake Bwana Nepi wakienda huku na kule wakiwafuata UKAWA eti kujibu mapigo kwa matusi na kejeli za kitoto!!! Katibu Mkuu mzima na akili zake anasema, ati KATIBA MPYA SI MUAROBAINI WA MATATIZO.....!!!!Kama huu siyo uhuni na matusi kwa Watz ni kitu gani??? Hivi Kinena na Nepi wanamdanganya nani asiyejua umuhimu wa KATIBA ambayo ndo sheria mama???
CCM na Serikali tunawaomba mjibu hoja na muache kejeli,mizaha na matusi kwa hoja nzito zinatolewa na Watanzania kupitia Wabunge wao wa Vyama vya siasa tofauti na CCM. Nje ya hapo ni kwamba mnajichimbia kaburi kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015.