CCM na Sera ya Tanzania Nchi Masikini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na Sera ya Tanzania Nchi Masikini.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Worshiper, Oct 19, 2012.

 1. T

  The Worshiper JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mrisho mpoto alisema katika moja ya mashairi katika wimbo wake mmoja "Mtoto akililia ndege inayopita angani baba humwambia asubiri kwanza itue akamletee ingawa anajua kwamba hata baiskeli hana".Hapa CCM(Serikali) ni kama baba wakati mtoto ni wananchi.Wananchi wengi wamekuwa wakiona rasilimali na utajiri mkubwa walionao (Ndege) vikinufaisha wengine na pindi wanapoinua kilio chao na madai juu ya rasilimali zao zinazotoroshwa,kuliwa na kufaidia mataifa mengine kila uchao huishia kudanganywa tu kwamba neema inakuja.

  Wakati huo huo huyu baba (serikali a.k.a CCM) anatoa ahadi ya neema kubwa (ndege kutua) kwa wananchi wakati yeye hana hata baiskeli (hapa ni mlinganyo wa faida inayopata serikali na rasilimali zinazotoroshwa) ambapo serikali hushindwa kutekeleza majukumu yake.Nchi imekuwa hainufaiki na rasilimali zake huku wananchi wake wakiendelea kuzama katika dimbwi la umasikini.Serikali ya CCM imekuwa ikitoa ahadi nyingi zisizo tekelezeka na kuwafanya wananchi kama watoto wadogo.

  Kauli za Tanzania ni nchi masikini zinazoimbwa na serikali ya CCM zimeshakuwa kero nakugeuka kelele zinazoumiza masikio.Uwezo wa serikali katika kushughulikia kero hii umeshaisha nguvu na ndiyo zimekuwa kauli zakudanganyia wananchi wakati wanadai haki zao za msingi.Kwasasa wananchi wanavyotaabika na umasikini na maisha magumu wakati watu wengine wanakuja kutajirikia hapa huku serikali ya CCM ikibariki siyo suala la kificho tena ni dhahiri.

  Sera mbovu na kufikia ukomo wa kiuwezo wa CCM katika kuongoza dola ni mambo ambayo yako wazi.Mikataba mibovu,kukosekana kwa mbinu na ubunifu katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika nchi ni janga la CCM.CCM imekuwa ikijitahidi kadri iwezavyo kila uchao kuwajaza kasumba hii wananchi kwamba Tanzania ni nchi masikini,na haisemi kwamba siku moja tunaweza kuondokana na hali hii.Ccm inataka kuwaaminisha wananchi kwamba hivyo ndivyo walivyo.Ukweli ni kwamba hata kama nchi isingekuwa na rasilimali zote hizo bado suala la maendeleo ni la lazima na nchi inaweza kuwa tajiri(ushahidi upo),ni mipango, ubunifu na ukombozi kifikra tu. Ni vyema kwa sasa Vyama vya upinzani vikawa na sera na slogan hii Tanzania ni nchi tajiri na kuifuta kabisa kauli ya uongo waliojazwa wananchi na kupandikizwa na serikali ya CCM.Kwani mapinduzi sahihi na ya kweli ya mtu binafsi,familia,jamii na taifa kwa ujumla huanzia katika kubadili fikra.
  Naomba kuwasilisha!!!!
   
Loading...