Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
'Malani',kadiri nijuavyo, ni maneno,mfananisho au kauli za kukwaza zinazoelekezwa kwa mtu fulani ili kumkasirisha.Malani si hoja ya msingi...ni kwa ajili ya kuudhi tu. Basi. Malani hasa hulenga mtu mwenye kumletea mtoa-malani changamoto mbalimbali. Ni hatua ya mwisho ya kushindwa. Mshindi kwenye malani huogopwa tu kwa umahiri wake wa kukashifu na kushambulia zaidi ya kujenga hoja. Hapati alama yoyote ya ushindi-kama mbunifu wa ustawi wa mtu au jamii. Sifa za 'kijinga' tu!
Sina uhakika kama CCM imeishiwa kazi za kufanya.Yenyewe ndiyo inayounda na inayoongoza Serikali ya Tanzania. Ina jukumu zito la kutekeleza Ilani yake ya mwaka 2010. Inahitajika,kila uchao,ije na hoja,ubunifu au utekelezaji wa Ilani yake. Lakini haipo hivyo. CCM sasa inamezwa na malani. Malani hayo yanaelekezwa hasa kwa chama kikuu cha upinzani nchini-CHADEMA.
CCM,inayotegemewa kuisimamia Serikali yake kuelekea ustawi wa Taifa hili, imetingwa na hoja nyepesi(malani) ambazo haziko hata kwenye Ilani yake na hata si njia ya kutekeleza Ilani hiyo. Nitoe mifano michache:
Kwanza,CCM iliibua suala la kadi ya chama hicho kumilikiwa na Dr.W.P.Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA. Ikasemwa kuwa Dr.Slaa anamiliki kadi ya CCM na anaendelea kuilipia. Wapo viongozi waliolipwa hata posho za chama kwenda sehemu mbalimbali za nchi hii kuhubiri habari hiyo 'njema' kwa chama. Hoja ikapuuzwa na wasikilizaji.Ikakimbiwa. Sasa imesahaulika.
Malani sasa yamehamia kwa John John Mnyika(Mbunge wa Ubungo) na Freeman Aikaeli Mbowe(Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni) juu ya elimu zao. Eti,mmoja form six na mwingine form four. Wapo makada wanapangiwa mikutano kuichagiza hoja hii. Wanahakikisha kuwa Waheshimiwa hawa wanasawajika kabisa na hawajiwezi juu ya hoja 'kali' kama hii.
Uongozi si elimu. Ni uwezo wa uchambuzi wa mambo,ubunifu,uadilifu na usimamizi wa kauli au matendo pamoja na nafasi ya kukubalika katika jamii. Ingekuwa elimu, viongozi wengi wa vyama vya siasa wasingekuwa na nafasi walizonazo hivi sasa. Elimu haimfanyi mtu kuwa kiongozi bora. Mnyika na Mbowe ni viongozi wa kupigiwa mfano Tanzania. Wanajitahidi kadiri walivyojaaliwa na Mwenyezi Mungu pamoja na kuwepo mapungufu yao ya kibinaadamu. Hawakufika hapo kwa elimu waliyonayo. Hata sisi wapiga kura tunapima vinginevyo na si elimu. CCM haina viongozi darasa la saba,Kidato cha nne na cha Sita?
Huu si muda wa malani...ni muda wa kustawisha nchi.Malani hayatawayumbisha walengwa.Yatawaimarisha zaidi.Yatayumbisha watoa-malani na chama chao. Wakipuuzwa na hapa,mchezo utakuwa mgumu mno!