CCM na Lowassa: Tathmini chungu ya kampeni za Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na Lowassa: Tathmini chungu ya kampeni za Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Baija Bolobi, Mar 31, 2012.

 1. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Wana JF

  Heshima zenu. Naandika maneno haya kutokea kwenye ngome ya CCM (Base), Gateway-Usa River.

  Ninafanya jambo hili kwa uzalendo kwa chama changu na taifa langu. Tuna mgogoro mkubwa wa ndani ndani, tunaomba msaada wenu. Naamini kwa kuvujisha mgogoro huu, tutaheshimiana huku ndani ili tumalize salama kampeini hizi za Arumeru Mashariki. Kuna masuala kadhaa hatukubaliani:

  -Lowassa amekuja kutudhalilisha: Tukishinda atadai ni yeye kasaidia tushinde, tukishindwa atadai alikuta tumeishaharibu kampeni na ndiyo maana tumeshindwa! Anatafuta sifa na ndiyo maana aliishia kusema yeye ni mtu wa vitendo, si domodomo - Kwani anagombea yeye?

  -Kuingia kwa Lowassa katika kampeini kumetugawa. Sisi tunaona hali yetu imekuwa mbaya zaidi na kuongeza kulaumiana badala ya kukabiliana na wapinzani wetu.

  -Katibu wetu wa Mkoa, Mary Chatanda hivi sasa anabanikwa eti anahujumu kampeni zetu kwa vile aliamua jana tufanye mikutano miwili badala ya mmoja; kisa? Mkutano wa Kikatiti ulikosa watu wa kutosha.

  -Lowassa hataki kukubaliana na tathmini yetu kuwa hali ni mbaya ili tukishindwa apate sababu ya kutushtaki kwenye NEC kuwa tulihujumu mgombea wake.

  Ni vema watanzania na wana CCM wakajua mapema tusije kulaumiana baadaye.
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwani TISS, polisi na NEC nao wameahidi kuwa betray? Ulivyoandika ni kama tayari hata huko hawataki watu wafe kwa ajili ya kumbeba mtu mmoja tena asiyekubalika hata na wanaCCM wenyewe.

  Ulivyotumia hiyo rangi nyekundu ni ishara ya maji kuzidi unga,


  Ona sera za CCM!!!!!!!!!
  Nipigeeeeeeee Nisipigeeeeeeee??????????????? ?????
  Pigaaaaaaaaaaaa
  Bendera ya CCM ina rangi ganiiiiiiiiiiiiii????????????? ??
  Kijaniiiiiiiiiiiiii.
  Ukipanda mahindi yanaota rangi ganiiiiiiiiiiiii???????????
  Kijaniiiiiiiiiiiiii.
  Ukipanda mpunga unaota rangi ganiiiiiiiiiiiiii???????????
  Kijaniiiiiiiiiiiiiiii
  Migomba yote ina rangi ganiiiiiiiiiii?????????????
  Kijaniiiiiiiii.
  Piga makofi na vigelegele kwa Chama cha Mapinduzi.
  CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeee.
  Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Sounds like a CHADEMA member pretending to be in CCM?
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kwanini umetumia red mkuu si ungetumia rangi za migomba!
   
 5. by default

  by default JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mkuu umetunga au ni kwel wamefikia hapa
   
 6. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Losambo
  TISS, POLISI NA NEC wamesema hawawezi kutubeba kama mazingira hayaruhusu. Kwa maoni yao, wanasema uchaguzi huu ni too close na kwa hiyo ni hatari kukurupuka kumbeba mtu.
  Jaji na Lubuva na timu yake wameweka kambi katika hotel ya NEW SAFARI HOTEL mjini Arusha na wamegoma kabisa kuonana na viongozi wetu wa mkoa na taifa isipokuwa kwa simu. Baadhi ya wasaidizi wa Jaji Lubuva wanatoka nje na kuonana na viongozi wetu lakini wanawaambia kuwa Mzee hapendi mchezo wa kubebana.
  TISS wameendelea kutusaidia kwa kutuletea habari za maeneo magumu huko vijijini na kutusaidia kununua shahada. Kutokana na mgogoro wetu wa ndani, tumejikuta tumenunua shahada hata za wapiga kura wetu wenyewe. Kutokana na ukata, wapiga kura wetu wanajifanya ni wana Chadema na wanauza shahada zao ili kupata fedha. Mabalozi walipoenda kuwatembelea usiku wakakuta wameuza shahada. Hii inatuchanganya.

  Kwa ujumla hali si nzuri sana na wala ujio wa Lowassa haujatusaidia sana zaidi ya kutuongezea mgongano wa ndani kwa ndani.
   
 7. M

  Mr Emmy JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,201
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Peleka utumbo na uharo wako huko CDM. Ndani ya chama cha mapinduzi hakuna mgogoro viongozi wakuu wametulia ndani ya kambi wakikamilisha mikakati ya ushindi na wengine tayari wameshafika katika eneo la king'ori kuratibu maandalizi ya hitimisho la Kampeni za Chama Kubwa lisilo na mpinzani CCM.
  Wana ccm wote Arumeru na Tanzania kwa ujumla msihofu ushindi upo upande wetu kwa tunakubalika na uwezo tunao CCM daima itatawala
   
 8. M

  Mr Emmy JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,201
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Leo Chadema mtapiga propaganda zote but CCM tumeshashinda. Kwani hivi sasa mitaa yote ya miji midogo arumeru imepambwa na kijani na wananchi wa rika zote wanaongelea ushindi wa kishindo wa CCM kesho hakuna zaidi ya hilo CCM ni zaidi ya uijuavyoo
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwani Siyoi ni mgombea wa CCM au wa Lowassa?!!!!!!!! Inabidi Tendwa avisajili hivi vyama ambavyo vimo ndani ya Magamba ili mambo yaeleweke. Magamba ni zaidi ya dampo la Tabata.
   
 10. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Lowassa ndio kioo cha CCM kwa wananchi. CCM ikishinda huko ujue ni kwa sababu wananchi wana imani na Lowassa.
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Wewe utakuwa ni mnafiki, na nyie ndio kikwazo cha Maendeleo katika Taifa letu, wewe weakness za chama chenu unakuja kuziweka hapa hadharani kwa faida ya nani? Unajenga chama au Unabomoa?

  Tabia hii iishie kwenye siasa zenu za kinafki ukizipeleka nyumbani kwako utapukutisha Familia nzima wewe.

  Na kwa maelezo yako inaonyesha kweli bila lowasa mlikuwa mmelowa sana, sijawahi kumsikia mpiganaji ambaye anawalazimisha wenzake kwamba hali ni mbaya, kama hali ni mbaya vitani inabaki salaha moja tu kunyanyua mikono juu, mbona haunyanyui mikono juu? nyie ndio watu ambao mko tayari kunyanyasika mpaka dakika ya mwisho kwa ajili ya shibe.

  Kwenye hiyo kambi yenu Lowasa ndiyo the only right person, hakuna kukubali kwamba hali ni mbaya, vita yenyewe hii haimtoi mtu roho unalalamika nini, Kaza masaburi upigane wewe alaaa.
   
 12. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna makao mazuri sana .......
   
 13. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  CCM kumekucha sasa
   
 14. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  CCM imeshindwa kwa hiyo hatuna Imani na Lowassa
   
 15. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Well said...
   
 16. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Naomba urudie kauli yako tena!
   
 17. kalukamise

  kalukamise JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 688
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Bangi rangi ganiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii???????????
  Kijaniiiiiiiiiiiiiii

   
 18. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  ...Kinyume chake ni kweli pia.
   
Loading...