Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,367
- 2,404
Jitihada za CCM kuivunja UKAWA kwa kuimega CUF kupitia Lipumba zimeshindwa. Mchezo huu umefahamika rasmi pale ambapo Msajili wa vyama bila aibu kuonekana kumkumbatia Lipumba kwa hali na mali.
CCM isichoelewa ni kitu kimoja, kuwa tatizo si CUF wala UKAWA, Bali wananchi wamebadilika. Hata bila ya CUF na ukawa vugu vugu la mabadiliko bado liko pale pale. Huu ni wakati mwingine, si wakati ule wa Nyerere, Mwinyi wala Mkapa. Vijana wanahitaji mabadiliko na ni lazima yaje.
Idadi ya vijana imeongezaka sana, halikadhalika idadi ya vyuo vikuu, mitandao, utandawazi, ambavyo hivi vyote huongeza upeo weledi katika mambo mengi ikiwa ni pamoja na demokrasia ambayo inaogopwa na utawala wa kidikiteta. Ni kweli, itayumba lakini mwisho wa siku wanachama wataelewa kuwa CUF ni muhimu zaidi kuliko Lipumba. Na huo ndio utakuwa mwisho wake.
CCM si pekee, vyama vingi vilivyoleta uhuru Afrika, kama KANU Kenya, cha Obote na cha Kwame Nkruma vilipitia njia kama hii ya ukandamizaji, fitina, kuwarubuni viongozi wa vyama pinzani kwa pesa na maneno makali kama "hatuondoki madarakani ng`oo n.k". Hizi ndizo dalili halisi ya vyama kama hivyo ikiwepo CCM. Hiki chama hakina miaka 10 kitapata kifo asilia.