MWANALUGALI
JF-Expert Member
- Feb 1, 2010
- 601
- 34
Mkuu mbona umeleta hoja ambayo haijadiliki, namaanisha ni hoja ambayo hiko obvious na kila mtu anaujua ukweli,
Mkuu hoja inajadilika, kama sijakosea CCM ambacho ni chama kilichoko madarakani kimekuwa kikishutumu vyama vya upinzani kuwa vina uroho wa madaraka ikiwemo chadema. Siyo mara moja au mara mbili, viongozi na wanaCCM kuipachika CHADEMA kuwa ni chama chenye udini na kwamba ni chama cha vurugu!! je haya hayawezi kujadiliwa? Humu JF hakuna watu wa kukisafisha CHADEMA au kuisafisha CCM kwa hoja? Nadhani kuwa tunaweza kuruhusu vichwa vyetu vikaanza kufikiri na kuonesha nani kati ya vyama hivi anacheza mchezo mchafu wa kuangamiza taifa letu!
Mkuu ninasema hii mada inamajibu tayari, ukiangalia hapo kwenye Nyekundu, Chadema si wa kwanza kupewa hizo sifa na cCM pamoja na serikali yake
CUF walipokuwa wapinzani wa kweli waliambiwa pia kuwa ni chama cha kidini, cha wapemba na pia ni chama cha vurugu, ilifikia mpaka IGP wa polisi (Mahita) kusimama mbele ya vyombo vya habari na kusema wamekamata Contena la CUF la zana kuulia (Majambia)
Ndio maana nasema majibu ya hii mada yapo open mno sioni cha kujadili
wa kujiangamiza ni sisi wenyewe
tunajiangamiza kwa kuchagua chama kisichokuwa na sera nzuri za kutuondoa hapa tulipo au tunajiangamiza kwa kutokuwaiga watunisia na wamisri??
chadema waache kufuata waraka wa kikatoliki ni hayo tu.
Tuache propaganda katika mambo makubwa yanayoweza kuangamiza Taifa, tujadili issues kwa makini tuone nani kati ya vyama hivi viwili anayetupeleka kusiko ili tuonye na kutoa ushauri kwa kuweka mbele mstakabali wa nchi yetu. Baada ya kuangalia mwenendo wa uchaguzi uliopita, tukaangalia mapokeo ya uchaguzi na mwenendo wa vyama hivi viwili baada baada ya uchaguzi, sasa tunaweza kujadili na kujiuliza Kati ya CHADEMA na CCM:-
- Nani anahatarisha usalama wa taifa letu?
- Nani mwenye uroho na uchu wa madaraka?
- Nani mwenye kutumia udini katika siasa zake?
- nani asiyekuwa na sera?
Unajua ndugu yangu hilo libambikiziwa na CCM ili kuweza kushinda ukweli sio huo. We angalia haohao wakatoliki mwaka 2005 walisema kikwete ni chaguo la mungu kwa vile leo wamewapinga CCM basi wanaiunga mkono CDM. Uwe na fikira nzuri ndugu yangu. Mbona 2005 walisema ni chama cha wachaga hilo leo halisemwi wewe huoni ni propaganda ?chadema waache kufuata waraka wa kikatoliki ni hayo tu.