CCM na CHADEMA mnatupeleka wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na CHADEMA mnatupeleka wapi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mmzalendo, Mar 3, 2011.

 1. mmzalendo

  mmzalendo Senior Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 165
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni miongoni mwana nchi tajiri kwa amani na utulivu, lakini kwa sasa
  hali inaoneka kuwa sio nzuri kutoka na msuguwano wa kisiasa kati ya chama
  tawala ccm na chama pinzani chadema.
  ccm wanasema chadema ni wachochezi, waloho wa madaraka pia ni chama
  cha watu wa kaskazini husani mkoa wa kilimangaro,
  chadema wao wanadai ccm wamezidi wizi wa mali za umma (ufisadi) na hawatufai
  wameongoza kwa miaka 50 hakuna cha maana chochote walichokwensha fanya mpaka sasa
  ukirudi kwenye hoja ya ccm kwamba chadema ni wachochote na kuinyumbulisha kwa undani
  unaweza kuibuka na mashwali kadha wa kadha
  mfano
  chadema ni wachochozi kwa mwelekeo upi? kuikomboa jamii au kuiangamiza? kwa maana
  hata baba wa taifa haliwai kuwa mchochozi wakati wa harakati za ukombozi kutoka kwa mkoloni, mimi
  ninsvyojua uchechozi ni kushawishi upande wako kukubaliwa na mwingine kuchukiwa na ili sio tatizo kabisa,
  kwa maana hiyo basi ccm wanatakiwa kujua kama serikali inakosea basi kukosolewa ni democrasia
  na wala hawapashwi kupiga kelele wala kuchagulia watu njia watakazotumia kuwapinga. ila wanatakiwa kuunga mkono ili kulinda masilahi ya taifa, maana uchechozi wowote unatoka na madudu wanayofanya viongozi wa serikali yake au waliyofanya huko nyuma
  Pia ukija kwenye hoja ya chadema kwamba ccm ni mafisadi na watumiaji vibaya pesa za umma,
  nadhani ili liko wazi na zaidi na ukweli wake sio wa kutafuta hata ,hali ya mtanznia ni ngumu na mawaziri na viongozi wengine wa ngazi za juu serikani wanaishi kama peponi kwa kutumia pesa ya umma, hakuna anayeshituka jinsi huduma za umma zinavyotolewa wala jinsi makampuni binafsi yanavyowaibia wananchi
  wazi wazi mchana kweupe. mfano bei ya sukari kupanda kwa sababu viwanda vimeficha sukari kwenye
  maghala yao kwa makusudi tu.
  hii hoya ni ya msingi lakini je chadema wana hakika gani kama ya mwembe chai au Arusha hayatajirudia tena?
  maana damu za watanzania umwagwa kila siku na police bia sababu.
  lakini ni kwa nini wasiwashitaki ccm kimataifa na kuwaelimisha wananchi
  umuhimu wa kura zao katika kuleta maendele, wakati wa uchaguzi wasimamishe wagombea wanaokubalika zaidi kwa wananchi na kwenye chama

  ndipo hoja na shwali la msingi ccm na chadema mnatupeleka wapi? je kuna anayejua kati yenu haya maandaki mnayoyachimba miyoni mwa wanatanzania yatafukiwa vipi? na hapa nina maana ya dhiki au kuchukiana wao kwa wao kwa kufuata vyama
  ccm kwa nini damu zinamwagika kwa visingizio vya juu juu tu? na chadema kwa nini msilekebishe harakati
  zenu kuokoa maisha yanayopotezwa na police wasio na huruma kila siku

  naomba kuwakilisha
  mdao


  source www.lifeofmshaba.com
   
 2. LUSAJO L.M.

  LUSAJO L.M. JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 223
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapa nadhani hoja sio Chadema na CCM wanatupeleka wapi ila tunatakiwa angalia kwanza mwelekeo wa Tanzania kama nchi kabla ya kuanza kunyooshea vidole CHADEMA na CCM na wapi wanapotupeleka. Tunatakiwa iangalia Tanzania kwa undani, wapi tunapotoka, wapi tulipo na wapi tunapoelekea kama nchi kwa ujumla.

  Katika hili tunatakiwa kuwaangalia tena viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza na tujiridhishe kama ni kweli wana nia thabiti ya kutuongoza na kuigeuza Tanzania kuwa ni nchi ya Ahadi, nchi ya maziwa na asali. Umenena vema kwamba Tanzania ni nchi yenye utajiri wa amani na utulivu lakini hali inaonekana kuwa mbaya kutokana na misuguano ya kisiasa kati ya vyama viwili vikuu vya siasa vilivyotajwa hapo juu.

  Tujiulize hapa je ni nini haswa ndio chanzo cha hiyo misuguano na ni nini ufumbuzi wa hiyo misuguano? Ukiangalia CDM ni chama kikuu cha upinzani Tanzania na kazi kuu ya chama cha upinzani ni kuwa "Watch Dogs" kwa serikali. Wanaiangalia serikali inafanya nini na kama ikiwa imepewa dhamana na wananchi kuongoza kama ipo kwa maslahi ya wananchi ama kwa maslahi ya wachache waliopewa nafasi kushika nyadhifa mbali mbali na umma wa Watanzania. Hoja zote ambazo CDM imekuwa ikiziibua ni za msingi sana na zipo kwa maslahi ya Watanzania zaidi lakini kinachotokea ni kwamba kwa kuwa CCM inayoongoza serikali inaichukulia CDM kama ni chama cha upinzani na kwamba hakuna zuri ambalo linaweza toka katika kambi hiyo basi wanaamua kuja na propaganda za uchochezi na uroho wa madaraka na udini.

  Tunapoongelea kwamba yasije tokea ya Mwembeyanga aus Arusha nadhani hapa you are missing the point that vyombo vya dola ndio vimekuwa mstari wa mbele katika kufanya mambo kama hayo yatokee. Sasa je tuna uhakika gani kwamba vyombo vyetu vya dola chini ya serikali ya CCM vitaendelea kusimamia kweli na haki huku vikitilia mkazo katika haki za binadamu katika kufanya yale ambayo ni haki zetu kimsingi zilizoainishwa katika Katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania?

  Kinachofanywa na CDM kwa sasa ni kuishtaki serikali kwa umma, tumekuwa tunarubuniwa kwa muda mrefu kwa kanga na tshirt na 'visenti' vidogo vidogo wakati wa kampeni za uchaguzi mpaka ikafikia tunakuwa vipofu katika machaguzi tunayofanya. Sio hayo tu pia mfumo mzima wa uchaguzi na vyombo vinavyoendesha vimekuwa vinatengeneza mianya mingi kwa chama kilicho madarakani kuvuruga uchaguzi kwa wizi wa kura na kuwaingiza madarakani wale ambao hawakuwa machaguo ya wananchi. Hili linalofanyika ni maandalizi ya mapinduzi makubwa ya utawala wa Tanzania, wanachofanya CDM ni kutoa elimu kwa wananchi na kuwafumbua macho wapate kuelewa maovu na mema ya waliopewa dhamana ya kutawala. Ninaamini ya kwamba ni mwanzo wa safari ndefu kuelekea mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli ifikapo mwaka 2015.

  Naamini CDM na CCM wanapotupeleka ni kwenye Tanzania bora inayoongozwa kimsingi na Utawala wa Sheria na Siasa safi. Naamini kwamba Watanzania wote tunasimama wamoja katika yale ambayo yanashusu zaidi maisha bora kwa Watanzania. Chuki zinazopandikizwa na uchochezi ni kati ya mbinu chafu zinazojaribu kuvunja nguvu ya mabadiliko inayokuja kwa kasi Tanzania. CDM wana haki ya kufanya maandamano na kuhamasisha wananchi kudai haki zao za msingi za kikatiba na wakati huo huo serikali inatakiwa kufahamu na kuja na njia ambazo zitaepusha umwagaji damu usio wa msingi. Serikali inatakiwa iangalie namna ya kuyapokea na kuyafanyia kazi yale yote ambayo CDM wanayapigia kelele. Lakini kama tutaendelea kuwa na serikali inayokazana kusema kwamba CDM ni wachochezi na wavunjifu wa amani huku wananchi kama mimi na wewe tunazidi kuumia....YATAFIKA.
   
 3. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Umenena, NIMEKUSIKIA NA JAMII ITAKUSOMA VEMA.
  Well said, nimependa ulivyochanganua.
   
Loading...