CCM na CHADEMA Dar wamgeuzia kibao JK

CCM na CHADEMA Dar wamgeuzia kibao JK

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Wafuasi wa CHADEMA waliongozwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambao walikuwa wakipeperusha bendera za chama chao na kuimba nyimbo mbalimbali huku wakidai maji. Hata hivyo, kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CCM waliungana na wenzao wa CHADEMA, kupiga kelele juu ya suala hilo kiasi cha kugusa hisia za Rais Kikwete.

Dar es Salaam. Ni nadra kutokea lakini wafuasi wa vyama vya siasa vya CCM na CHADEMA, wameungana kumweleza Rais Jakaya Kikwete kuhusu kero ya maji eneo la Kimara-Golani, Dar es Salaam.

Rais Kikwete alikutana na hali hiyo wakati akifungua Daraja la Kimara jana, tukio hilo liliwakusanya watu wengi hasa wanachama wa CCM na CHADEMA waliokuwa wamevalia sare za vyama vyao.

Wafuasi wa CHADEMA waliongozwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambao walikuwa wakipeperusha bendera za chama chao na kuimba nyimbo mbalimbali huku wakidai maji. Hata hivyo, kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CCM waliungana na wenzao wa CHADEMA, kupiga kelele juu ya suala hilo kiasi cha kugusa hisia za Rais Kikwete.

Akizungumza baada ya uzinduzi wa daraja hilo, Rais Kikwete aliahidi kuitisha kikao Jumatatu ijayo kitakachomhusisha Profesa Maghembe na maofisa wa wizara yake, wabunge wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa, wakuu wa wilaya ili kuweka mikatati ya pamoja kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

"Ninaomba Machi 25... tukutane ili tuweke mikakati ya pamoja kutafuta ufumbuzi wa suala hili," alisema Rais Kikwete.

Akiwa Hospitali ya Mwananyamala, Rais Kikwete alizindua maabara ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi na akazungumzia suala la dawa za kulevya kwa kusema atahakikisha mapambano yanaendelea kwani dawa hizo zinaua nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana.

Source: Mwananchi
 
Kuweka mikakati!! Mhhh... Kwani hakuna mikakati.... Au sijasoma vizuri? Isiwe kuna watu wanataka kukimbia vivuli vyao hapa.
 
Kwani chadema imeahilisha maandamano ya tarehe 25.03, sasa mbona mnyika anaitwa ikulu wakati atakuwa kwenye maandamano..
 
Wafuasi wa Chadema waliongozwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambao walikuwa wakipeperusha bendera za chama chao na kuimba nyimbo mbalimbali huku wakidai maji. Hata hivyo, kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CCM waliungana na wenzao wa Chadema, kupiga kelele juu ya suala hilo kiasi cha kugusa hisia za Rais Kikwete.

Dar es Salaam. Ni nadra kutokea lakini wafuasi wa vyama vya siasa vya CCM na Chadema, wameungana kumweleza Rais Jakaya Kikwete kuhusu kero ya maji eneo la Kimara-Golani, Dar es Salaam.
Rais Kikwete alikutana na hali hiyo wakati akifungua Daraja la Kimara jana, tukio hilo liliwakusanya watu wengi hasa wanachama wa CCM na Chadema waliokuwa wamevalia sare za vyama vyao.

Wafuasi wa Chadema waliongozwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambao walikuwa wakipeperusha bendera za chama chao na kuimba nyimbo mbalimbali huku wakidai maji. Hata hivyo, kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CCM waliungana na wenzao wa Chadema, kupiga kelele juu ya suala hilo kiasi cha kugusa hisia za Rais Kikwete.

Akizungumza baada ya uzinduzi wa daraja hilo, Rais Kikwete aliahidi kuitisha kikao Jumatatu ijayo kitakachomhusisha Profesa Maghembe na maofisa wa wizara yake, wabunge wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa, wakuu wa wilaya ili kuweka mikatati ya pamoja kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

"Ninaomba Machi 25... tukutane ili tuweke mikakati ya pamoja kutafuta ufumbuzi wa suala hili," alisema Rais Kikwete.

Akiwa Hospitali ya Mwananyamala, Rais Kikwete alizindua maabara ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi na akazungumzia suala la dawa za kulevya kwa kusema atahakikisha mapambano yanaendelea kwani dawa hizo zinaua nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana.
Source: Mwananchi

huyu JK ama kweli ni bonge la msanii, hivi haelewi kuwa March 25, ni siku ya msiba wa taifa kuililia elimu Tanzania, aambiwe hicho kikao apange tarehe nyingine bana. Mnyika si alikuwa hapo kwa nini hakumkumbusha kuwa hiyo tarehe ina tukio la kitaifa nchi inakwenda kusimama ili kujitafakari kuhusu elimu na mengineyo.
 
Nahisi jambo la busara ni kusubiri tarehe ifike ili tuangalie nini kitafanyika, ikiwa hawakuitwa na hakuna lolote lililofanyika hapo ndipo tuzungumzie usanii
 
Atahakikisha mapambano ya madawa ya kulevya yanaendelea!!? mhhhh haya!!
 
Atahakikisha mapambano ya madawa ya kulevya yanaendelea!!? mhhhh haya!!

Aisee rais wetu huwa na guts, kwa kutoa ahadi na maneno matamu kusikia, mtu aweza pata na mhemuko akidhani ghafla bongo itakuwa London!
 
ccm walijua kofia na kanga zitawaletea maji, wamegundua matatizo hayachagui ccm wala chadema..dawa ni kuungana na wapigania maendeleo bila kujali itikadi za kisiasa!!
 
Hawa ccm ndio wanachelewesha maendeleo kwa ushabiki wa kijinga hata kwenye matatizo ya msingi.
 
Tarehe 25. March Waziri mkuu mpya wa CHINA anakuja kusaini mikataba 11 ikiwamo GEC ya Riz1 Mtwara. Siku hiyohyo Mnyika ataenda Ikulu kujadili hoja ya maji ambayo "Bi Kiroboto" na Naibu wake "Ndugu yai" walizigomesha Bungen. SIKU HIYOHIYO NCHI ITASIMAMA, KULILIA ELIMU YETU. Ni makusanyiko ya AMANI kumsihi Kawambwa na Mlugo watuachie ELIMU YETU. VIVA CDM
 
Tarehe 25. March Waziri mkuu mpya wa CHINA anakuja kusaini mikataba 11 ikiwamo GEC ya Riz1 Mtwara. Siku hiyohyo Mnyika ataenda Ikulu kujadili hoja ya maji ambayo "Bi Kiroboto" na Naibu wake "Ndugu yai" walizigomesha Bungen. SIKU HIYOHIYO NCHI ITASIMAMA, KULILIA ELIMU YETU. Ni makusanyiko ya AMANI kumsihi Kawambwa na Mlugo watuachie ELIMU YETU. VIVA CDM.
 
tarehe 25. March waziri mkuu mpya wa china anakuja kusaini mikataba 11 ikiwamo gec ya riz1 mtwara. Siku hiyohyo mnyika ataenda ikulu kujadili hoja ya maji ambayo "bi kiroboto" na naibu wake "ndugu yai" walizigomesha bungen. Siku hiyohiyo nchi itasimama, kulilia elimu yetu. Ni makusanyiko ya amani kumsihi kawambwa na mlugo watuachie elimu yetu. Viva cdm.

wanasiasa wanaweka mikakati wakti issue ni bomba bove na mitambo ya kizamani
 
Back
Top Bottom