CCM na ACT watupiana mawe Korogwe

CCM na ACT watupiana mawe Korogwe

Nas Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
5,286
Reaction score
5,423
Wakuu poleni na shughuli zenu za kujitafutia mkate,

Nimechelewa kuleta taarifa hii kutokana na sababu mbalimbali,siku ya jana majira ya mchana kumetokea vurugu baina ya wafuasi wa ACT na CCM,ikumbukwe kua jimbo la Korogwe lipo chini ya CCM kwa miaka mingi ambapo kwa sasa wanamgombea wao Mery Chatanda,

Uchaguzi huu umekua na upinzani wa hali ya juu kwenye jimbo hili hasa baada ya Salma Mtambo kujiengua CCM na kujiunga ACT ambapo kwa sasa nae yumo katika kinyang'anyiro hicho cha ubunge,wamama hawa wananguvu sana eneo hilo,sikubahatika kuona tukio mpaka mwisho ili kupata undani wa vurugu hizo ingawa baadhi ya mashuhuda wanadai wafuasi wa CCM walikwenda kwenye kambi ya ACT na kuanza kurushiana maneno jambo ambalo lilipelekea kutupiana chupa na mawe.

Maoni binafsi: Wanachi wenzangu tuacheni siasa za visa maana kuna maisha baada ya uchaguzi.
 
Baba na mwana hao, watakatiwa mirija ya kampeni mama Ngwila(Nkwila kwa kifipa au mnafu kwa wale wa dar) asitishe kampeni. Wanakorofisha bosi
 
Baba na mwana hao, watakatiwa mirija ya kampeni mama Ngwila(Nkwila kwa kifipa au mnafu kwa wale wa dar) asitishe kampeni. Wanakorofisha bosi

mkuu hawa act si kuna kipindi tulisikia mzee edo ndio mdhamini au tulidanganywa?
 
Hii ccm ya kishenzi hii imeanza lini?? Ninaomba viongozi wa juu wa ccm wakemee tabia ya wafuasi wao kufanya uchokozi na kuanzisha vurugu wakidhani wako juu ya sheria.

Kumbukeni kwamba wananchi hawatutaki na kwamba tumesalia wachache. Wakiamua hawa kutumaliza, hata jeshi halitatuokoa zaidi ya kulinda watawala na majengo.

Ccm viongozi waambieni wafuasi wenu wafuate sheria na waheshimu uvumilivu na utulivu wa halil ya juu unaoonyeshwa na vyama vya upinzani. Wasije wakadanganyika kwamba ukimya wa upinzani ni woga!.

TUTAKWISHA WATABAKI WANAOLINDWA NA MAJESHI TU KINA JK NA FAMILIA YAKE.
 
Nyie si mnasema Act ni ccm sasa mnalia nini unafki tu.

swissme
 
mkuu hawa act si kuna kipindi tulisikia mzee edo ndio mdhamini au tulidanganywa?

Mlidanganywa na Mbowe kumbe Chadema na Mbowe mlikuwa mnakula pesa za Edo na Rostam tokea 2011
Poleni!
 
Act ni ccm B. Viongozi wa juu ndo hadwa Ccm B wengine wote wanaburuzwa tu.
 
Act ni ccm B. Viongozi wa juu ndo hadwa Ccm B wengine wote wanaburuzwa tu.

napata wakati mgumu sana kuelewa hili jambo before mlitusminisha kua lowassa ndie mfadhili leo hii act mwatuambia ni ccm b aaaah which is which
 
Baba na mwana hao, watakatiwa mirija ya kampeni mama Ngwila(Nkwila kwa kifipa au mnafu kwa wale wa dar) asitishe kampeni. Wanakorofisha bosi

mkuu hawa act si kuna kipindi tulisikia mzee edo ndio mdhamini au tulidanganywa?

Aah wapi mkuu Walidanganya tena sana, tena mbona inajulika wazi kuwa hata mshahara wa ZZK unatoka Lumumba wee hujui jamaa zetu akina "Goli la Mkono' kwa viini macho na mambo yao kupumbaza umma. Na hao ACT wameshaingizwa mkenge saa hii tayari wako juu ya mawe chali bila msaada kwani kazi yao imeshakwisha wakiwa wameshindwa kuparaganya kura za UKAWA kama malengo ya ilivyotengenezwa.
 
Back
Top Bottom