CCM mwisho wao umekaribia, Ole kwa wale waliowaibia watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM mwisho wao umekaribia, Ole kwa wale waliowaibia watanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pax, Sep 7, 2010.

 1. P

  Pax JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Dalili zote zinaonekana ule mwisho wa CCM hatimaye umekaribia. Watanzania wengi wameamka, wanajua haki zao kuliko kipindi kingine chochote sasa. Wakati wa watu kuwasikiliza watu kama wakina Makamba na Kinana unaelekea ukingoni, wakati wa kupata kura kwa kuongea upupu na kutoa ahadi zisizotimizika umekwisha. Ati mgombea anasema sijui Kigoma itageuzwa kuwa Dubai, jamani vioja vingi mwaka huu. Watu hawana hata barabara unawaambia habari za uwanja wa ndege?vituko.

  Wanamageuzi nchini pote msikate tamaa, jamii ya wapenda haki ipo nyuma yenu. Watu wamefikia mahali wanarithisha wajukuu zao uongozi ka vile watu wengine hawapo. Tumenyanyasika, tumeibiwa, tumepigwa kiasi cha kutosha. Hatuwaachii sasa hivi, mwisho wenu umekariabia, tunakaba mpk mkose hewa, mkose pa kukimbilia.Tukikamata nchi tunawaondolea kinga ya kushtakiwa, kizimbani mtapanda mkikutwa na hatia, ole wenu kama mmewaibia maskini hawa wa Tanzania.

  Tunasema ole wenu, maana ule mwisho umekaribia, ole wenu.
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kigoma kuwa Dubai labda walikuwa wanatania
   
 3. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama chukizo la Uharibifu wa CCM limeshaingia kwa Watanzania basi ule mwisho umekwisha fika
   
 4. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  CCM wametenda dhambi kubwa sana kwa watanzania, kwa kuuharibu mpango wa Mungu kwa taifa letu. Mpango wa Mungu wakati anaiumba dunia ni kuwa sisi watanzania tuwe jamii ya watu waliobarikiwa saaana kwa kutupatia utajiri mkubwa wa rasili mali kuliko nchi yoyote hapa duniani, Mungu alitaka watanzania tuwe matajiri. Lakini leo hii watanzania ndiyo watu masikini kuliko wote duniani, chanzo cha umasikini wetu ni utawala mbaya uliochia rasilimali zetu zikombwe usiku na mchana bila ya sisi kuambulia kitu.Na waliotutawala kwa miaka hamsini hii ni CCM, hivyo hawawezi kukwepa lawama ya KUWAFUKARISHA WATANZANIA KINYUME CHA MPANGO WA MUNGU.Kwa vile wametenda dhambi lazima mauti iwakute kwani mshahara wa dhambi ni mauti.Nazungumzia mauti ya kisiasa, lakini ikibidi hata mauti ya kimwili kwa wooote waliowafukarisha watanzania hawana haki tena ya kuishi
   
 5. D

  Dopas JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huu mwisho tunausubiri kwa hamu kubwa. Hakuna utawala usio na mwisho. Hasa utawala wa kifisadi na kidhalimu tena unaangamia vibaya. Siku hiyo ikifika itakuwa kilio na kusaga meno kwa kina Makamba, Abdul Kinana na wezi wenzao.
   
 6. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kigoma kuwa Dubai inawezekana kama tutaambiwa au kuoneshwa ni kivipi kwa kila namna kuanzia Fedha... na potential nzima ya mpango huo wa kuifanya kigoma kuwa Dubai kama kuHAMIA Dodoma iMESHINDIKANA TOKEA UHURU hadi leo..

  Pia inaonesha uwezo wa kufikiri na kufikiria kati ya wagombea na wapiga kura... may be ni bora ahadi na mengineyo yanajulikana au kujulikana baadae kwamba Kikwete hagombei tena 2015 sasa nani wa kumuuliza ahadi zake ziko wapi...?

  Inafaa iwekwe sheria ya kuwabana watoa ahadi wakati wa kampeni kama wakishindwa kuzitekeleza na kama hawako tena madarakani waweze kufikishwa mahakani na kujibu au kutiwa hatiani na kufungwa kwa kipindi kisichozidi miaka mitano tangu wakati wa kampeni ulipopita.. maana wamewadumaza na kuwahadaa electorate kwa ahadi ambazo hawakuzitekeleza...
   
Loading...