CCM Mwanza wamuweka mtegoni Magufuli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mwanza kimemtaka Rais John Magufuli kuwatimua kazi Marry Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Kiomoni Kibamba, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, kwa kukaidi maagizo ya chama hicho wakati wa kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga,

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu Rais Magufuli aagize wakuu wa Wilaya za Nyamagana na Ilemela jijini hapa kusitisha zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara hao katika maeneo ya katikati ya Jiji.

Rais Magufuli aliagiza machinga kuendelea na shughuli zao katikati ya Jiji mpaka pale uongozi wa jiji hilo utakapotenga maeneo ambayo ni rafiki, huku akidai wanaweza kufunga barabara moja ili machinga hao wafanye biashara zao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mustapha Banigwa, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Nyamagana, amesema kuwa kabla ya zoezi la kuwaondoa machinga hao, Oktoba 25 mwaka huu Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ilikutana na kuzuia mpango wa Mkuu huyo wa Wilaya.

Banigwa aliyazungumza hayo kwa niaba ya chama hicho, mkoa wa Mwanza, huku akidai kuwa pamoja na kamati hiyo ya siasa kumshinikiza DC Mary Tesha kuacha utaratibu wa kuwaondoa machinga lakini alikaidi na kuendelea kusimamia uamuzi wake.

“Kitendo cha DC na Mkurugenzi wa Jiji kukaidi maagizo ya chama kinadhihirisha dharau na kiburi. Tunamuomba Rais Magufuli atengua teuzi zao na kuteua watu wenye uwezo wa kuwatumika Wananchi.

DC na DED wanafanya mambo bila kulishirikisha Baraza la Madiwani na hata Meya wa Jiji tulipomuuliza anasema suala hilo hawakushirikishwa,” amesema Banigwa.

Aidha Banigwa ameeleza hofu ya chama hicho kupoteza majimbo ya Nyamagana na Ilemela ikiwa wateule hao wa rais hawataondolewa.

“Rais aangalie maslahi mapana ya wananchi wa Mwanza, akiacha hawa watu waendelee na kazi kwenye wilaya zetu, tutakuwa tunaelekea kupoteza majimbo. DC na DED lazima pia warejeshe fedha Sh. milioni 180 zilizotumika katika zoezi la kuwaondoa machinga katikati ya Jiji,” amesema.

Hussein Kimu, mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Nyamagana, amesema maamuzi yaliochukuliwa na viongozi hao, yamekifedhehesha chama hicho na wao kama vijana katika wilaya hiyo walipinga zoezi hilo lakini walishangaa kuona machinga wakiondolewa katikati ya Jiji.
 
Hii tena ni fitna.Kuna utendaji.kuna sheria,kanuni na taratibu za mipango miji.
MKUU WA NCHI,alichofanya ni siasa,na hawa viongozi wa chama wanaleta tena siasa.
Mwanza ni mji ambao unamapungufu,kutokana
na makosa ya miaka ya nyuma(kuacha wananchi kujenga kiholela hadi mlimani,na washukuru tetemeko halikupiga mwanza,tungeona maafa ambayo hayajawahi kutokea).
Ahadi ya rais kuifanya Mwanza kuwa mji wa kisasa haitotimia,kama viongozi wataendekeza siasa!
Siku za nyuma miji na majiji yalishindanishwa kwa usafi,hili viongozi wa kisiasa wanasahau!,na sheria ni kwa wote sio inapofika
wananchi wamekosea tupindishe sheria.
Tutajenga taifa la wananchi wasio tii sheria(manajiamilia kujenga maeneo ya hifadhi ya barabara,na mabondeni,na kujichukulia sheria mikononi).
Ili tuendelee nidhamu iwepo miongoni mwa wananchi na hata viongozi.
Sasa sehemu kubwa katika jamii haitaki kufanya kazi,imekuwa ni stori za vijiweni na kulalamika kila siku.
 
Yote haya yanatokana na uchaguzi ndani ya CCM mwakani na machinga wamekuwa wakitumika kama mabango ya wanasiasa hapa nchini. Wafukuzeni hao mnaopendekeza, lakini bado machinga wataondolewa mara uchaguzi utakapomalizika.
 
Mkuu wa mkoa aliyajua yote na ndiye aliyekuwa nyuma ya mpango wote
DC ni mbuzi wa kafara tuu
 
Yaani kumbe CCM huwa wanashinikiza katiba,sheria na kanuni zisifuatwe?

Kumbe inawezekana hata Zanzibar kwa jecha lilitokea shinikizo!

Kumbe hata arusha labda lilitolewa shinikizo!

Hakika mmejianika kwamba huwa mnashinikiza mambo yenu kwa maslahi ya kisiasa

Chama.kiko juu ya sheria za mipango miji? yaani juu kiko chama na ilani,chini kuna sheria,ikitokea mgongano wa sheria na chama,matakwa ya chama yanazipiga kumbo sheria!!
 
Naungana na chama cha mapinduzi kuwa viongozi hao walikiuka agizo la mh. Raisi, lakini sikubaliani kuwa teuzi zao zitenguliwe, labda wahamishwe na kupelekwa wilaya zingine
 
Halafu baada ya hapo watageuka na kudanganya kuwa rais anafuata sheria na kila mtu anatakiwa atii sheria bila shuruti! Hiihii nchi kwenye miji yetu mikubwa, kuna watu wanakamata magari na kutoza faini kubwa kwa kisingizio cha wrong parking, lakini katika miji hiyohiyo na barabara hizohizo kuna wajasiriamali na wafanyabiashara wanafungua 'maduka' yao pasiporuhusiwa na sheria za barabarani na kumbe wanatetewa... tena na watawala! ccm + uongo na unafiki ni damdam!
 
Back
Top Bottom