nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
[h=2]
[/h]JUMATANO, JULAI 11, 2012 06:24 NA JOHN MADUHU, MWANZA
WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, wamemtuhumu mwenyekiti wa chama hicho mkoa, Clement Mabina kuwa ni mmoja wa viongozi wanaokiangusha chama chao.
Mabina, alishushiwa tuhuma hizo nzito katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho, kilichofanyika Chuo cha Veta Nyakato, kilitawaliwa na maneno ya kejeli,vurugu na ubabe, huku baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakitishiana kutaka kupigana ngumi kavu kavu kutokana na kutofautiana kauli.
Wajumbe wa kikao hicho, inaelezwa walikuwa wakitofautiana na wakati mwingine kuzomeana au kupigiana makofi kutokana na tofauti zilizopo.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zinasema tuhuma za Mwenyekiti kujihusisha na rushwa na kushindwa kukiongoza chama hicho na kukisababishia kupoteza baadhi ya majimbo zilirushwa kwake na wajumbe wa Halmashauri ya Mkoa, Richard Rukambura pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athuman.
Taarifa za uhakika, zinasema aliyeanza kumshambulia Mabina ni Rukambura ambaye alikieleza kikao hicho kuwa suala la kupinga rushwa katika chaguzi limekuwa zito kutokana na viongozi waliopewa dhamana ya kupiga vita rushwa wamekuwa wakijihusisha na rushwa.
Tuanze nawe Mabina,wewe ni mpokeaji wa kitu kidogo namba moja,umekuwa ukipokea rushwa katika chaguzi mbalimbali kwa ajili ya kuwapendelea baadhi ya wagombea,hivyo hufai kuendelea kuwa Mwenyekiti",alisema Rukabura.
Kutokana na madai hayo, alikuja juu na kumtaka mjumbe huyo aketi chini ambapo hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu, Kache aliingilia kati na kumtaka Mabina kumuacha mjumbe huyo azungumze suala hilo hadi mwisho.
Kiongozi mwingine, aliyemtuhumu Mabina ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athuman alidai mwenyekiti huyo ameshindwa kuunganisha chama.
Akijibu tuhuma hizo, Mabina aliiambia MTANZANIA kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake hazina msingi wowote, zaidi ya wajumbe hao kuwa na chuki zao.
Haya ni mambo ya kupangwa ili kuvuruga kikao,mimi sio mla rushwa, nafuata taratibu katika kusimamia haki na sio vinginevyo",alisema Mabina