CCM mwaka huu NGANGARI kinoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM mwaka huu NGANGARI kinoma

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Sep 6, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,197
  Trophy Points: 280
  WATU wanaoaminika kuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kijiji cha Sengenya wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki iliyopita waliwazingira na kutaka kuwapiga viongozi wao waliokuwa katika kikao, kutokana na madai ya kutoridhishwa na matokeo ya kura za maoni za nafasi ya ubunge zilizompa ushindi Dunstan Mkapa.

  Watu hao wanadaiwa kutaka kufanya hivyo wakati chama hicho kikiwa katika harakati za kuwanadi wagombea wake, huku kikiwataka walioshindwa katika kura za maoni kuvunja makambi ili Chama hicho kiibuke na ushindi mkubwa.

  Kabla ya kuzingirwa, viongozi hao ambao ni wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Chibwana Mtimbe, Mkapa na aliyekuwa mpinzani wake katika kura za maoni, William Dua na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Alhaji Dadi Mbullu waliwasili Kijiji cha Sengenya Ijumaa iliyopita saa saba mchana.

  Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wananchi hao walianza kuwazomea viongozi hao huku wakipinga kufanyika kwa kikao hicho kijijini hapo kwa madai kuwa viongozi hao wameshiriki kumpa ushindi Mkapa badala ya Dua waliyeamini kuwa alishinda katika kura hizo.

  “Wananchi walianza kwa kuzomea, mara baada ya msafara huo kuingia kijijini hapa, baadaye walijikusanya na kuanza kuwarushia mawe…kama sio polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi, sijui ni nini kingetokea,” alisema mmoja wa mashuhuda hao ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

  Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mtwara, Alhaji Mbulu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa maelezo ya kina anayo Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo.

  “Ni kweli jaribio hilo limetokea ila itakuwa vyema ukiongea na Katibu wa Wilaya ya Nanyumbu….kama kuna mambo utahitaji ufafanuzi zaidi ninaweza kujazia hapo,” alisema Mbullu.

  Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Mohamed Kateva licha ya kukiri kuwapo kwa jaribio hilo, alishutumu watu waliofanya vurugu hizo na kuwaita kuwa ni ‘wahuni’ ambao sio wanachama wa CCM.

  “Naweza kusema ni wahuni…sisi tulikwenda kwa nia ya kuvunja makundi yaliyojitokeza katika mchakato wa kupata mgombea, ubunge na udiwani, wao wanadhani mgombea wao alishinda na kulikuwa na hila ya kumnyima haki yake.

  “Ni utaratibu wa Chama kuvunja makambi kabla ya kuanza kampeni ili kukinusuru Chama, wale wanachama tulikaa nao na kufanya mkutano lakini hao wahuni wakafika na kuanza kurusha mawe, tulitoa taarifa Polisi na kuomba ulinzi na kama sio polisi tusingetoka kwa urahisi,” alisema.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Its good inaonyesha wananchi wanavyotaka kuwa na Viongozi bora na si kubebanabebana tuuu! wananchi toa mafisadi woote kwa nguvu zooote!! ccm inatakiwa isafishwe na si kupeana vyeo kama machiefu.
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,375
  Likes Received: 3,138
  Trophy Points: 280
  Ilimradi kaonesha kuutaka uongozi basi kwa mujibu wa kikwete hata akikosa bado zipo nafasi nyingi tu za wale makapi ambao wananchiu wamewakataa...asihofu Mkapa kikwete kamwandalia ukuu wa mkoa/wilaya hao wanaokupinga wajutaa kukujua......hii ndiyo ccm bwana yaani ngangali kuliko hata cuf
   
 4. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Hamna ungangali majizi tu!!
   
 5. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  he he he heeeee
   
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  MIAKA YOTE NGANGARI kinoma:becky:
   
 7. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  kidumae chama cha majambazi
   
 8. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,197
  Trophy Points: 280
  Mwaka huu mmechukua nafasi ya CUF udaku nyie ngumi nyie nasikia juzi mmevunja kioo gari la mpiga debe wenu sijui mtambembelezaje mzee wa kiraracha.
   
 9. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  AAH wapi sisi sio wale tuliotaka kuwapiga waandishi wa habari.. :becky:
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Sep 7, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  This is one of the rare opportunity where the opposition could make the difference! the question is, are they keen enough to seize the opportunity!! to turn the fracas into fortune. remain to be seen.
   
Loading...