CCM Mtwara wamtetea mbunge Ghasia. Wasema mama aliyemshukia mbele ya Rais Magufuli alitumika kisiasa

Mar 22, 2019
46
55
Na Bakari Chijumba, Mtwara.

Chama cha mapinduzi(CCM), Wilaya ya Mtwara vijijini,kimeeleza kusikitishwa na kuhuzunishwa na kitendo kilichofanywa na mmoja wa wananchi wa Nanguruwe ambaye alimueleza Mh.Rais Joh Pombe Magufuli kwamba ni kama vile hawana mbunge na wamewahi kutembelewa mara moja pekee na mbunge huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama cha mapinduzi wilaya ya Mtwara,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mtwara vijijini Nashir Mfaume, amesema Chama hicho na wananchi walio wengi wanautambua mchango mkubwa ambao Mbunge Ghasia ameutekeleza katika kukuza maendeleo baada ya kupewa ridhaa ya kuwa Mbunge.

Nashir ametoa takwimu za ziara ambazo Mh.Hawa Ghasia amekuwa akizifanya katika kata ya Nanguruwe tangu mwaka 2016, ambazo zimonekana kufikia zaidi ya 11 huku akisimamia miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Billion 1.5 katika eneo hilo la Nanguruwe.

"Tumehuzunishwa na kitendo cha mwananchi wa Nanguruwe,kumueleza Rais Magufuli kwamba hawana Mbunge na hajawahi kuwatembelea..Mh.Ghasia amesimamia miradi ya maendeleo ya zaidi ya Tsh.Billion 1.5 Nanguruwe na ametembelea zaidi ya Mara 11" amesema Nashir na kuongeza kuwa;

"Jimbo la Mtwara vijijini lina vijiji 110 na kata 21 lakini yeye tangu 2016 ametembelea zaidi ya mara 11 Nanguruwe pekee, ambapo katika eneo hilo kupitia mfuko wa jimbo wa mbunge na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo serikali, Mbunge Ghasia kwa kipindi tu cha mwaka 2015-2018 amesimamia jumla ya miradi ya maendeleo yenye thamani ya Tshs.1,577,340828.26."

Aidha mwenyekiti huyo wa CCM wilaya amewataka wananchi kusoma alama za nyakati na kusema mtu anaweza kuhoji vitu kwa kuwa tu anatumika na watu kwa sababu mbalimbali ikiwemo za kisiasa, na kuongeza wao kama chama wamemuomba Mbunge atulie na hasijibu lolote.

"Sisi Kama chama,pia wananchi wanajua mchango wa Mh.Hawa Ghasia,mtu anaweza kuhoji vitu kwasababu ametumwa pasipo kujua dhamira ya kutumika huko kuna maana gani, hata ninyi waandishi mkifika Nanguruwe na kukagua vitabu vya wageni mtathibitisha ukweli wa namna Mbunge Ghasia alivyotembelea Nanguruwe..Tumemwambia Mbunge atulie,asijibu kelele hizo,CCM tunalifanyia kazi,tutawaletea majibu kilicho nyuma ya Pazia"

Kwa upande wake Katibu wa siasa na uenezi CCM wilaya ya Mtwara Selemani Sankwa, amewasihi wanaotaka nafasi za udiwani na ubunge kusubiri wakati muafaka badala ya kutengeneza kile alichokiita mbinu za kuwadhoofisha walio madarakani

"Kama katibu wa siasa na uenezi CCM wilaya(Mtwara),nimesikitika yule mama sijui katumwa na nani!,kusema mbunge Ghasia hajawahi kufika Nanguruwe..Nitoe wito kwa wanaotaka ubunge na udiwani,wawaachie viongozi waliopo wafanye kazi,watakaokaidi panga litawapitia 2020." amesema Sankwa

Mama mmoja mkazi wa Kijiji cha Nanguruwe, alimshutumu Mbunge wa Mtwara Vijijini Bi.Hawa Ghasia kutotembelea eneo lao na kuhamishia ujenzi wa makao makuu ya Wilaya kwenye kijiji cha Mkunwa badala ya eneo hilo,jambo ambalo lilikanushwa na Mbunge huyo mbele ya Rais Magufuli na kusema tatizo la Nanguruwe ni Hosptali ya wilaya ambayo ilihamishiwa Mkunwa, jambo lililopelekea Rais Magufuli kuagiza ujenzi wa Hospatali hiyo uendelezwe hapo hapo Nanguruwe.
IMG_20190408_131044.jpeg
IMG_20190408_131047.jpeg
IMG_20190408_131050.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao viongozi hawajitambuli, mbona kwa kumwaga mboga hadhari kwa mwanamama huyu kumeweza kurudisha ujenzi wa Hospital hapohapo Nanguruwe? Huyu mbunge alijificha wapi kipindi chote hicho, yaani miaka minne ametembelea mara 11, yaani ni mara 3 kwa mwaka.
 
Pamoja na hayo hiyo ni alert kuwa jina lake halitarudi 2020 mana ni maji na moto akipata kifuta jasho chake pale mjengoni awaze cha kufanya asitapanye kwa kutaka kurudi tena ni maoni yangu tuu!

Hakuna aliyewahi kuwa waziri wa JK masikini - Ghasia anatengenezewa sababu ya kumwengua - kambi bado zinawatesa baadhi ya watu
 
Pamoja na hayo hiyo ni alert kuwa jina lake halitarudi 2020 mana ni maji na moto akipata kifuta jasho chake pale mjengoni awaze cha kufanya asitapanye kwa kutaka kurudi tena ni maoni yangu tuu!
Mmmmmm usimutishe bhana. Acha ajaribu tena ubunge mtamu asikwambie mtu.
 
Back
Top Bottom