Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,760
Kila Mzanzibari alie CCM ambae ni kiongozi anaeonekana kwenda kinyume na matakwa ya CCM mwisho wake huwa mbaya na huvuliwa nyadhifa zote za uongozi na kutupwa kama mzoga na huonekana si lolote si chochote katika jamii ya wanaCCM. Na hili zaidi hutendewa WaZanzibari tu ,angalia Akina Seif na wenziwe wakati wa Nyerere walitimuliwa ,ni juzi tu Mansor Yousef nae katimulia ,hata haukujatulia Yule Mwanasheria Mkuu nae anaundiwa zengwe afukuzwe habari zipo huku Othman Masoud kufukuzwa nafasi ya MMWZ na Kupewa Mkusa Sepetu..Bado iko siri - Mzalendo.net
Mbona huku Tanganyika hakuna afukuzwae kuna mambo kibao ,hatusikii Mtanganyika kufukuzwa lile la Mwigulu kama angelisema Mzanzibar ndani ya bunge la Katiba bai ingelikuwa ameshapata la kumpata ,mbali ya viongozi wakuu waliohusishwa na mambo mbalimbali ikiwemo rushwa na mikataba mibovu kama wangekuwa wazenji wangelikwisha fukuzwa chamani na kutolewa ndani ya serikali .ila tunawaona akina Lowasa wavijisenti. wanapeta ndani ya CCM mbali waliojitangaza kugombea uraisi ndani ya CCM ,kama wangelikuwa wazenji basi wangekwishatimuliwa.