Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,858
Mwanzo mwanzoni,natamka kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania wala kwingineko. Na wala sijawahi kuwa mwanachama ingawa nina ndoto za kuwa mwanasiasa.
Chama tawala CCM,wakati Katibu Mkuu akiwa Wilson Mukama, kiliweka mpango wake wa kujivua gamba. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ndiye mwanzilishi wa msemo huo wa kujivua gamba,CCM ilidhamiria kuwapoka vyeo na hata kuwatimua wanachama mafisadi waliopo CCM.
Katibu Mkuu wa zamani wa CCM Wilson Mukama angalau alikuwa akisemea jambo hili ingawa limeshindikana kutekelezwa kwakuwa hakuna taarifa rasmi ya kichama. Katibu Mkuu wa sasa wa CCM Kinana na hata chama kwa ujumla kimekuwa kimya juu ya kujivua gamba.
Falsafa ya Rais Magufuli anayetokana na CCM ni kupambana na wizi na ufisadi. Yeye anawavua magamba watumishi wa umma kwa njia ya kuwatumbua majipu kama anavyopenda kuiita. Katika falsafa na matendo haya ya Rais Magufuli,CCM imepata nafasi ya kumuunga mkono katika kusafisha chama kwa njia ya kuvua gamba. Hakuna haja kusubiri hadi yeye awe Mwenyekiti.
Hii ni nafasi ya CCM kujisafisha kama kweli ina nia ya kupambana na ufisadi kupitia Serikali inayotokana na chama hicho.