Mwamba Usemao Kweli
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 744
- 186
CCM mpya Tanzania mpya
Hayawi hayawi sasa yanaenda kutimia...Tunahesabu masaa kuanzia leo kabla ya tarehe 23.7.2016 ambapo nchi mpya inaenda kuzaliwa. Ni nchi yenye jina lilelile Tanzania ila yenye mtazamo, utamaduni wa kutenda na utashi mpya katika kusimamia maendeleo ya watu wake na njia zake kuu za uchumi inaenda kuundwa.
Naona mabadiliko makubwa katika utumishi wa umma, jumuia na shughuli za mtu mmoja mmoja unaenda kusimikwa na kuanza kutumika kuwezesha uzalishaji mali wenye tija na maslahi katika nchi yetu, maeneo husika ni pamoja na:-
1. Viwanda na uzalishaji
2. Kilimo
3. Uvuvi
4. Madini
5. Mifugo
6. Misitu na nyuki
7. Teknolojia, elimu na utafiti
8. Utalii na maliasili
9. Biashara ya ndani na nje
10. Ujenzi
10. Elimu
11. Siasa na jamii
12. Sheria na usimamizi wake katika kupambana na rushwa na ufisadi.
13. Ulinzi na usalama wa nchi yetu
Maeneo tajwa na mengineyo mengi yaliyo sahaulika kwa pamoja yanaenda kupewa msukumo mpya ndani ya Tanzania.
Rais wetu Magufuli ni tunu ya kipekee kabisa ambayo watanzania tulimuomba mungu na hatimaye ametupatia. Tumpe ushirikiano. Wapo watakao umia katika utekelezaji wake lakini hakuna njia nyengine kwani siku zote dawa/matibabu ya ugonjwa sugu huwa yana changamoto nyingi.
Watanzania tujipange nchi hii ni tajiri na inauwezo wa kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Tumuunge mkono mheshimiwa J.P.J Magufuli.
CCM mpya na Tanzania mpya chini ya J. P. J. Magufuli.
Mungu ibariki tanzania.