JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,114
- 3,541
salamu wanabodi!
Mwanzoni nilimuunga mkono mheshimiwa JPM kwa hatua mbalimbali alizo kuwa anachukua ili kuiweka Nchi vizuri.Nikasema, naam haya ndio mambo ambayo sisi wapinzani tulikuwa tunayataka.Kuna watu walikuwa wananiambia hapana ni mapema mno kumsifia mtu huyu! Na kweli ndivyo ilivyo geuka na kuwa ni mtu asiye aminika hata kidogo.Dalili ya mvua ni mawingu.
Katika kipindi kifupi siyo tu kwamba amevunja katiba ya Nchi bali pia inaonekana huwa haisomi kabisa na wala hana mpango huo.Yeye ndio kila kitu.Sijui kama anapata muda kuwauliza watangulizi wake jambo lolote!
Wito wangu kwa CCM, wakati wa kutumia busara, hekima, maarifa na maono ndio sasa. Kuna kila dalili kwamba huko tuendako Nchi yetu itaangamia.Huwezi kuwazuia watu kufanya siasa wakati wewe unafanya siasa halafu watu wakakubali wakakaa kimya! Huwezi kuwahukumu wazee kwa kuwaambia hawaaminiki halafu wote tukamwamini yeye mtu mmoja. Hatari zaidi ni kumpa mtu madaraka yote ya Nchi huku mkijua ni mwepesi wa kulipa visasi! CCM hamtabaki salama hata kidogo.Salama yenu ni kutenganisha madaraka! Kinyume cha hapo hamta baki salama.
Mungu amesha waonesheni kila dalili. Nani hajaona? Ni juu yenu CCM kukilinda chama chenu au kukiangamiza.Hivi ninyi mlioko ccm inawaingia akilini kwamba miaka michache iliyo pita Nchi yetu pamoja na Nchi zingine chini ya Umoja wa mataifa tulipeleka vijana wetu Nchini DRC kupambana na kikindi cha M23, ambacho kila mtu anajuwa wanaungwa mkono na Rwanda halafu kabla hata ya kuondoa vijana wetu huko, kiongozi mkubwa anasema yeye ni Rafiki mkubwa wa Kagame? anajua kuwa anawapa wakati mgumu vijana wetu?
Chukueni tahadhari, jipeni muda wa kutosha kupima mambo kwa faida ya Nchi.Mambo yanayo husu masilahi ya Nchi ni vizuri kila mmoja wenu akawa kwenye kiwango chake bora kabisa cha kusema ndio kama jambo ni jema na kusema hapa kama kuna kila dalili kuwa huko tuendako tutaangamia.
Hatuwezi kukaa kusubiri maendeleo kwa kuharibu demokrasia. Demokrasia ambao ndio uhuru wa asili wa binadamu yeyote huwezi kuiuza ili upate maendeleo.Tunataka kiongozi anae heshimu Katiba ya Nchi n kuitii kwa vitendo.
Kila la heri CCM, ila kama nauona mwisho wa chama chenu, chukueni kila tahadhari, itisheni mjadala mpana wenye uhuru kamili kwa faida ya chama chenu.