CCM mnaniita mnyonge, mmeninyongonesha tangu mnichukue kwa mkoloni. Niwapende kwa lipi?

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wakati tukijiandaa kupata baraka la kupuliza kipenga cha ufunguzi wa kampaini za kuomba ridhaa ya kuongoza tena

Bado nafikiria hawa watu CCM waliokabidhiwa nchi kutoka kwa mkoloni mweupe nao wakajigeuza mkoloni mweusi kwa kutenda mabovu tuliyokuwa tunamwimbia mkoloni mweupe aondoke atuachie ardhi yetu. Huku tukifunga na kuomba mzungu huyu aondoke kwa amani bila kumumwaga damu kama walivyofanya wenzetu Kenya na Zanzibar. Sasa huyu mkoloni mweusi kabla mzungu ajafika mbali ndiye kaja na mateso zaidi. uteka yeye , kutesa yeye, kunyima haki yeye, kufunga watu midomo yeye ,kunyanganya mali yeye. Kufungia mgazet yeye. Kumbuka mkoloni mweupe alitujengea reli, viwanda bandari lakini bado tulimkataa, katujengea mahospitali mashule lakini katunyima Uhuru. Tunaishi kwa wasiwasi , simu zetu za kuteta hata jambo jema linadukuliwa. Tunaishi kama mafisi. Hivi cccm ulizaliwa nakuona nikakuomba uniongoze ni utoe huu unyonge wa kijinga nilioingizwa kwa mtutu wa bunduki na mkoloni mweupe.

Mwanangu CCM kwani nilikufanyia nini hadi kuninyima usingizi hivi, unanilaza na njaa hata nashindwa kununua sukari. Hizo barabara pekee za kukupitisha wewe uwahi kunikama kwa sababu ya kusema ukweli hazitakusaidia kama sisi wajumbe na wanyonge tukiungana kukuondoa wewe mkoloni mweusi. Mmejitayarisha na kuunda makundi mengi ya wasanii kuja kutuonyesha sanaa zao huku tukiwajua kwa saana kwamba manyimbo yao yamejaa matusi, yamevuka tamaduni. Kukaa uchi wao, kuimba nyimbo mbovu za kuiga toka kwa mashetani wao.

Siwakatai sana kwa sababu wengi wametikea kwenye familia za malezi haba. Ninachojua wanakuja kutupigia kelele tuu wakiondoka wajumbe na wanyonge tutanongonezana na tujue la kufanya.

Mwanangu CCM sikio LA kufa ndilo hili unyonge tunaweza kuoondoa kwa hiari kupitia kura si kwa kutulazimisha kwa vitisho mpaka yuke mkoloni mweupe anakushangaa kwani wakati unadai utatutendea vyema hukufnya hivyo. Umeleta mateso hadi yeye anakuonya kila Siku na mabarua kibao. Hakujua kama ungebadirila kuwaumiza masikini wenzake, angejua angelibaki

Mlitunyonga kwa kamba Nene hatukufa tuliweka mikono yetu Mungu akatupa hauweni, sasa kwanini wewe uliyejigeuza adui tusikumalize? Tulikuwa tunakupenda sana CCM , tukakupa muda ujirekebishe ukaibuka na matusi unatuita maskini! LA sasa tumejielewa maji utayaita mma
 
Mkuu usikubali kuitwa mnyonge aisee ni upuuzi mtu,
NB: yani nikisikia mtu anasema jpm ni rais wa wanyonge namuangalia namusikitikia sana...

Tayari hii virus wamekewa kichwani mwao ya kwamba ni wanyonge.
 
Mkuu usikubali kuitwa mnyonge aisee ni upuuzi mtu,
NB: yani nikisikia mtu anasema jpm ni rais wa wanyonge namuangalia namusikitikia sana...

Tayari hii virus wamekewa kichwani mwao ya kwamba ni wanyonge.
Sipendi kuitwa mnyonge wala maskini wakati Nina akili timamu, na viungo vyote vya binadamu, namtafuta yule anayenilazimisha kunitia umaskini ili aniite mnyonge
 
Back
Top Bottom