CCM mnamtafuta Gorbachev wenu?

Unajua hata maana critical thinking
Critical thinking ni CCM kuongeza idadi ya risasi kwaajili ya wahuni kama wale wakijitokeza tena. China wanafanya hivyo, NKorea wanafanya hivyo, Urusi wanafanya hivyo na Cuba wanafanya hivyo. Bila CCM imara nchi itayumba. Hebu ona sasa hivi vurugu zilitokea watu walikufa, mali ziliharibiwa lakini nchi iko imara na mifumo yote iko intact na watu wako wamoja. China haibembelezi wakora, Nyerere alikuwa habembelezi wakora, Castrol alikuwa habembelezi wakora, Jong Kim Un habembelezi wakora na Putin habembelezi wakora. Tz tunajisifu hatuna ukabira wala udini kwasababu wa uimara wa Nyerere. Yaani Kambona alikiona, Jumbe alikiona, Bibi Titi alikona, Maalim alikiona, G55 walikiona, Salmin na kila mtu aliyetaka kutikisa kiberiti alikiona cha mtemakuni.

Mfumo huu wa ujamaa na kujitegemea hautaki kiongozi legelege anaekenua sana.

China wanakwambia wao ni 25% ya watu wote dunia kama utaruhusu kila mtu atukane hovyo mitaani utamsikiliza nani. Viongozi wao waulize wachina zaidi ya 1b watakula nini, watakunywa nini, watalala wapi, watatibiwaje, watasomaje na watavaa nini badala ya kuwauliza demokrasia ambayo haisambazi maji kwa watu 1b.
 
Lumumba itabakia Pango tupu.
Kumbe wewe hujui kitu. CCM ni jeshi na jeshi ni CCM, hata sasa CCM imedhoofika lakini CCM itaendelea kushinda tu. kwani wewe unadhani kule Rwanda, Uganda, Burundi vyama tawala vinashinda uchaguzi miaka yote hiyo?. Waafrika na Waarabu hawahitaji demokrasia bado, bado wanahitaji kuambiawa nini wafanye na nini wasifanye. Ndio maana unaona mpaka leo kuna kaya hazina vyoo, vijana mchana wanacheza pool na kuishi kwa shemeji. bado kuna mtu anadhani uchawi na maombi vinaweza kumpatia mali. Watu wamejazana kwa Mwamposa na wengine bado wanakata viungo vya albinos kusaka utajiri, watu kama hao demokrasia inawasaidia nini?
 
Unaandika uchafu.
Ccm imeshinda uchaguzi mara ya mwisho mwaka gani ?
Hayo ya uhawi anza na hao sisiem wenzio majuha kabisa kutwa kushindana kwa waganga then unakuja kuandika upumbavu kama huu.

Huu ni unafiki wa kuwapaka Rangi watu waliojaa uchafu wa kila aina.

Huku kupinda pinda kwenu mnafanya tuwe na mashaka hata na jinsia zenu.
 
CCM kwa sasa haina haja ya kushinda uchaguzi, inashindana na nani? Jukumu la CCM kwa sasa ni kuwahakikishia wananchi wote bila kuwabagua amani, utulivu, usalama wao na mali zao, kuwapa huduma na kuvilea vyama vya upinzani mpaka vikomae na kuwa tayari kushindana na CCM kwa hoja, sera na mipango ya kuijenga nchi yao.

Tume ya uchaguzi haina haja ya kuengua wagombea hata wakikosea ili angalau wawe wengi bungeni na serikali za mitaa. Mwl. NYERERE alivitaka vyama vya upinzani vianzie bungeni sio Ikulu baada ya kuviona bado havijakomaa kiasi cha kukabidhiwa nchi. Aliviita "the dogs"; I cant let the country go to the dogs. Maana wenyewe kama watoto wanapinga kila kitu na wanasema hadharani kila kitu bila kuhifadhi siri za nchi yao. Wanadhani wazungu ni watu wema kwao na kwa taifa. Ni rahisi kuiuza nchi ilimradi wafike Ikulu bila kuwa na sera wala mipango yoyote. Wao ni Ikulu tu baasi, wakifika watajua hukohuko.

CCM haihitaji kiongozi anaeona haya kuilinda Katiba hii kama ilivyo, na kuiambia dunia sisi tuko hivi mkitaka haya mkikataa haya. Hakuna kuwa vuguvugu (in between).

Sisi ni wajamaa dunia lazima ijue hivyo, wananchi wetu hawauwezi full ubepari. Lazima huduma za msingi za umma ziimarishwe kwaajili ya watu wote. Shule na hospitali za umma ziwe bora kuliko au kama za private maana sisi ni wajamaa bado. Hatuwezi kuwa na katiba ambayo hata mlevi na kuwadi anaweza kupenya na kufika Ikulu; tumekwisha.

Utakuta mtu anadai demokrasia na Katiba mpya kwa nguvu wakati huohuo amehodhi eka 300 za ardhi ya kabila lingine. Mzanzibar anadai muungano ufe huku amahodhi eka 1000 Morogoro, watoto wake wamejaa mtaa wa shaurimoyo DSM wanauza spare za magari kama watanzania wa kawaida tu. Ni ulevi tu.
 
Huu utamaduni ni kwa maslahi ya taifa, Chama ,maslahi ya wananchi, maslahi ya wanachama au maslahi ya viongozi wakuu wa CCM ?
Kaka huu utaratibu ndio unaotupatia reli, barabara, umeme kila kijiji, maji, hospitali, shule, mikopo ya elimu, madaraja marefu na amani na utulivu bila kubaguana kwa kabila, dini wala kanda. Hivyo faida ni kwa taifa zima.
 
Communisty party ya china, mtu au kiongozi akifanya ufisadi ananyongwa, akila rushwa anafungwa, Je CCM watayaweza hayo?
Hilo ni tatizo, Nyerere alitukosea hapo. Alikopi Katiba ya China lakini akaacha usimamizi mkali wa viongozi. Hapa pia lawama ziende kwa Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa kuja na Azimio la Zanzibar lililolegeza maadili ya viongozi.

Mimi hapa kama ukiniambia tufanye marekebisho ya Katiba ningekwambia tuongeze kifungu kinachowanyonga viongozi wakuu wala rushwa, wezi, wabadhilifu, wanaovunja muungano, wanaotaka Tanganyika, wanaohubiri udini na ukabila na wanakibeza Kiswahili na kutaka lugha zao za kienyeji zitumike. Mambo hayo yawe ni uhaini.
 
Mkuu kuna mambo mengi umeyasema ni mazuri but kuna mangine hayana afya.Kuna mambo huwezi kuyazuia kwa kuyahairisha yataleta balaaa huko mbeleni lazima yatafutiwe ufumbuzi.Marais waliotangulia kushindwa kuyatatua sio kwamba ndio mtu asiweze kuyatatua.
Mfano mdogo kabisa wakati wa nyerere na hata kikwete miaka ya majuzi hapo kulikuwa na fair katika uchaguzi,na wabunge wa upinzani walikuwa wanaongezeka kila mwaka kwa nini kwa Magufuli wapungue.

Ni kweli Kikwete na Samia wanaogopa nchi na Chama kufia mikononi mwao,but ni kipi ufanye.Ukiangalia model ya Russiq sasa hivi vyama ni kama ni mfu-lazima ukubali kupoteza.Huko China unapopatolea mfano mfumo wao wa uongozi upo imara sana ndio maana wapo vizuri kiuchumi.

Ukweli mchungu ni kuwa Magufuli na Lisu wamisha iua CCM yetu,ni ngumu na jambo lisilowezekana kumsimamisha mgombea wa CCM na upinzani free & fair ashinde.
 
Ni mfumo tu watangulizi/babu na bibi zenu wameshaamua kwaajili yenu hakuna kihoji. Huwezi kuhoji kwanini wewe una jina hilo, una dini hiyo au una kabila hilo. Babu na baba yako waliamua kwaajili yako. Kule Uingereza pamoja na ukongwe wao na usomi wao na werevu wao lakini babu zao waliamua kuwe na ukoo mmpja tu wa kifalme unaowatawala kama mazuzu na wala hawahoji kwani familia moja tu itutawale na tuilishe milele. Kule Marekani babu zao walishaamua kuwa ni nchi ya muungano na namna ya kumpata Rais na ubepari ndio mfumo wao, na hakuna anaeruhusiwa kuhoji kwanini wanapiga kila mtu na kunyang'anya mali za wengine kibabe kama vile walivyofanya Venezuella, Iraq, Libya, Chile, nk

Pale Kenya babu zao tayari waliwaamulia kwamba nchi yao itaendeshwa kibelpari, na hakuna anahoji hilo, akihoji mtu kwanini ardhi yao yote inamilikiwa na watu wachache atakiona au kutekwa apotee.

Hata sisi hapa tayari babu zetu Nyerere, Karume na waliokiwepo wakati huo walishaamua kwaajili yetu kuwa hakuna Tanganyika, kuna muungano na ujamaa na kujitegemea ndio mfumo wefu.

Kazi ya kiongozi ni kueleza na kufundisha vizazi na vizazi kuhusu maamuzi hayo ya babu zetu ambayo lazima yafuatwe litoke jua inyeshe mvua. Katiba yetu hii ndiyo inayotutofautisha sisi na mataifa mengine, lazima ilindwe kwa nguvu zote hata kama sio nzuri kama ya Marekani. China wanalinda Katiba yao hata kama wapo wasiokubaliana nayo.

Vyama vya upinzani vikitaka viende Ikulu haraka lazima vikubaliane na Katiba hii kama ilivyo maana hii Katiba ndiyo inayotufanya sisi tuwe hivi tulivyo. Chama na mgombea kama atapinga Katiba, muungano hawezi kuachwa ashinde uchaguzi hata kwa kibiwa kura zake, hafai na hatufai. Hata Marekani au UK hakuna mgombea atasema muungano wao US au UK haufai nikishinda nitaurekebisha ili kuleta usawa. Mgombea wa hivyo atakamatwa.

Mpaka sasa wapinzani wanashindwa uchaguzi hawaibiwi kura. Hakuna mtu anaeweza kuiba kura nyingiiii za mgombea. Wapinzani mpaka leo hii wanavizia watu wanaoachwa CCM ili wawe wagombea wao ubunge na Urais. Walifanya hivyo kwa Dr. SLAA, MREMA, LOWASSA, MEMBE, SUMAYE, MPINA, NK kuonyesha kuwa upinzani bado kabisa uko rojorojo. Hiwezi kuniambia Lissu ambae hata kwao Ikungi hawamtaki anaweza kuwa Rais wa nchi hii, labda kwa kukinukisha.
 

Bado sana bob kaza mimi nimeshatoka kwenye fikra za watu akili kama zako watu tuko mbali na hawaamini kama tuko mbali sasa wewe endelea kushinda na dunia wanasema dunia haitasimama ukigoma kutembea nayo
 
Communisty party ya china, mtu au kiongozi akifanya ufisadi ananyongwa, akila rushwa anafungwa, Je CCM watayaweza hayo?

Huyu hajui chochote ni watu flani ambao wanajiona wana akili kumbe hopeless
 
Communisty party ya china, mtu au kiongozi akifanya ufisadi ananyongwa, akila rushwa anafungwa, Je CCM watayaweza hayo?
Watanyogwa wote waishe hadi wakosekane wa kuwanyonga wengine
 
Bado sana bob kaza mimi nimeshatoka kwenye fikra za watu akili kama zako watu tuko mbali na hawaamini kama tuko mbali sasa wewe endelea kushinda na dunia wanasema dunia haitasimama ukigoma kutembea nayo
Sisi tayari mambo yetu, tunakisemea kizazi cha vijana na watoto ambao hawawezi kumbambanua. Hata hivyo haya ni maoni yangu tu, hasa kutokana na exposure yangu iliyotukuka na elimu ya kuunganisha dots.
 
Mmmmh !! 😳
Ngoja Tusubiri tuone !
Wazanzibari nao ?! Wanasemaga vipi ?!
Wamechoka kuburutwa ?! 🀣😁😳 !

Kazi kweli Kweli ! πŸ˜€πŸ€£
 
Kweli wewe ni mjamaa na wajamaa tunajua kuandika kweri kweri!
 
Kweli wewe ni mjamaa na wajamaa tunajua kuandika kweri kweri!
Kiongozi anaeona haya kuilinda Katiba aliyoapa kuilinda hatufai leo hata kesho na keshokutwa. Katiba yetu hairuhusu kupokea maagizo kutoka EU au Marekani maana viwango vyetu havifanani kabisa, na tulisema hivyo punde tu baada ya uhuru. Sisi viwango vyetu ni vile vya China na Urusi, na ndivyo vilivyotuletea heshima hii tunayotamba nayo kuwa tulikuwa nayo huko nyuma. Ni upumbavu kudai Katiba kama ya Kenya au nchi za EU. Yaani mjinga anakwenda kushitaki uchaguzi wetu EU; sisi sio wa EU, Kenya sawa. Sisi tuulizwe habari za China maana babu zetu wa Taifa Nyerere na Karume walikuwa na fafiki yao ambae ni mchina, Mwenyekiti Mkuu Mao ambae aliwafundisha mambo mengi ikiwepo mavazi yasiokuwa na shingo (kola), na siasa zetu, ingawa wao wakasema hawataki kufungamana na upande wowote.

Ujamaa huu tayari umeshatuingiza hasara kubwa lazima tuendelee nao tu milele. Mfano, ujamaa huu umeruhusu makabila mengine kwenda kutwaa na kumiliki ardhi za wengine zilizotunzwa vema na babu zao kwaajili ya watoto, wajukuu na vitukuu vyao vijavyo. Leo hii msukuma anamiliki eka 3000 kwenye ardhi ya wafipa bure kabisa halafu msukuma huyohuyo anasema Katiba hii iliyompatia ardhi ya makabila mengine haifai tunaandamana. Kama hivyo lazima warudishe ardhi ya watu kwanza kisha wainunue kwa bei ya kibiashara (kibepari).
 
Hata Xi Jinping na Putin wamepewa more time kutokana na umuhimu wao, sisi hapa hapana kwanza, ingawa tunao ushahidi kuwa marais wanaume ni ama wezi au wabadhilifu au vyote kwapamoja.
 
Kweli wewe ni mjamaa na wajamaa tunajua kuandika kweri kweri!
Naandika kwa uchungu kaka. Hii Katiba na huu muungano hadi kufika hapa vimeumiza watu wengi sana. Kuna watu walipoteza, kufungwa, kuumizwa, kukimbia nchi na wengine hata kufa kabisa ili Katiba na Muungano udumu milele. Hawezi kutokea mtu mmoja au kundi likasema Katiba haifai na muungano huu haufai kuwa hivi. Huyu mtu wa hivi lazima akumbane na hasira kubwa.
 
Vijana wa leo hawajui tumetoka wapi! Tutaulinda Muungano wetu kwa gharama yoyote ile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…