CCM mnajua ubovu wa katiba ya sasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM mnajua ubovu wa katiba ya sasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamakabuzi, Nov 22, 2011.

 1. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nimeshangaa sana kuona wabunge wa CCM wakishupalia na kupitisha muswada wa mchakato wa marekebisho ya katiba. Kilichonishangaza ni kwamba sijawahi kusikia mbunge wa ccm akisema katiba ya sasa ina ubovu fulani na hivyo inahitaji kurekebishwa au hata kuandikwa upya! Wabunge hawa wamepitisha muswada ambao hawajui unakusudia kurekebisha kasoro gani katika katiba ya sasa. Ni wazi kama hawaoni kasoro zilizopo, watatunga sheria itakayoendeleza yaliyopo.
  Kwa mfano kuna tunaoona kuwa katiba ya sasa ubovu wake mkubwa ni kumpa rais madaraka makubwa sana ambayo hayawichecked na chombo kingine tofauti; sisi wenye muono huo tunaona muswada uliopitishwa juzi bungeni umeendeleza hayo hayo ya rais kupewa madaraka makubwa sana kwenye mchakato na hivyo kuzaa katiba itakayoendeleza hayohayo.
  Je wewe mwana ccm unaweza kutuambia ubovu unaouona katika katiba ya sasa na kutuonyesha kuwa mchakato unaowekwa utaondoa ubovu huo?
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na hiyo ndiyo maana halisi ya kuwa na presidential system of governance. Powers are vested in the President and there are checks and balances such as the Parliament. Sasa wewe unachozungumzia ni kitu tofauti. Muswada ulikuwa umpe Rais madaraka kwa sababu unaakisi kilichopo katika katiba ya sasa. Lakini hayo haimaanishi kwamba katiba ijayo itakua hivyo kwa sababu wananchi watakuwa na fursa ya kuchagua mfumo wa utawala wanaoutaka na huo utawekewa misingi madhubuti ya udhibiti ili kusiwe na excesses au abuse. Lakini hiyo ni hatua ijayo ambayo hatujaifikia na unashangaa kelele hizi ni za nini. Ni kama kisa cha Lwekamwa na kuchukizwa na rangi ya katiba na kuamua kuisigina.
   
 3. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Asante kwa mchango wako; hoja ya msingi katika thread ni je ccm wanajua ubovu wa katiba ya sasa? Kama hawaujui (ubovu) then watatengeneza katiba kama ile ile tu.
  Pili hayo madaraka makubwa ya rais ni kweli muswada umeakisi yaliyomo kwenye katiba ya sasa; je ni lazima muswada huu umpe tena rais madaraka hayo; hakukuwa na njia nyingine kwa mfano ya kuunda tume? Namna tofauti ya kupitisha hadidu za rejea? Namna nzuri zaidi ya kuteua wajumbe wa bunge la katiba? nk. mpaka yote yafanywe na rais. Je katiba ya sasa imetoa utaratibu huo katika mchakato wa kuibadili?
  Waswahili husema nyota njema huonekana asubuhi!. Kama unataka kwenda mashariki halafu unachukua barabara inayoelekea kusini, hakika hutafika mashariki hadi utakapogundua kuwa umepotea na kuamua kurudi uanze upya.
  Hiki ndicho kinachotekea; rais ana madaraka makubwa sasa na anayafurahia na wana ccm wenzake (ndiyo maana ccm hawajawahi kusema katiba ina ubovu), leo unapompa madaraka makubwa tena kwenye mchakato, unategemea aunde kitu kitakachopunguza hayo madaraka yake?
  Nahifadhi kumbukumbu hii hadi katiba mpya then we will see!
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  naona wanachelewa kujibu, ni kuwa hawajui!!!
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo watatumia hela yetu lakini mwishowe wataturushia katiba yenye madudu yale yale!
   
Loading...