CCM Mnajilinda bila ulinzi

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,993
Reaction score
34,867
Wakuu,

Nimetafakari sana nguvu kubwa na ya makusudi inayotumika kuidhoofisha kabisa Chadema tena wahusika hawana tena hata soni waziwazi.

Haya yote lengo kuu ni kukilinda chama tawala, lakini huu ulinzi mbona hauna ulinzi? Public awareness kwa yanayoendelea mbona ni sawa na kuzungusha ukuta na kuweka mageti makubwa bila kuyafunga?

Ndio tunajua CCM haitotawala milele lakini jinsi Chadema inavyoshughulikiwa kwenye jicho la umma ni sawa na mtoto yatima anayenyanyaswa na kupigwa huku akikatazwa kulia. Watu wanaona mnawapuuza mnaamini mnawamudu.

Hatari itayowakabili ni siku hizo thermometers zenu zitapowaambia joto ni 36 degrees kumbe ni 98 degrees. Hamtaamini tatizo ni thermometers au macho yenu.

Acheni taasisi za kiraia zitimize wajibu wao na ionekane hivyo na kila mmoja aamini hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…