CCM mna laana, Elibariki Kingu alivyochorwa na CAG Ufisadi wa 101M

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,090
114,628
CCM mme laaniwa, mnaiba hela katika ngazi zote za nchi hii, mnaiba kuanzia ngazi za wizara mpaka mashinani,mpaka kimataifa kwa kuanzisha makampuni hewa ya kimataifa ya kuibia hela.

Leo nawaletea udondozi wa ripoti ya CAG huko Igunga Tabora , kuna mambo yamnistua. Hivi wizi ndio sifa kwa CCM kumpa mtu cheo?Kwa ufisadi ninaousoma hapa kwenye repoti ya Hamashauri ya Igunga, basi Elibariki Kingu, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo na baadae kuwa mbunge wa CCM Singida,inasikitisha na kutia hasira.

Halamshauri imepata hati ya mashaka……………..CAG anasemaje katika ripoti yake? Yapo mengi, mengine zungumza wewe mimi najikita kwenye ufisadi wa SHS.101,174,585 unaomuhusu Mbunge huyo moja kwa moja.

1. Imepigwa milioni 95 fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana

Katika ripoti ya CAG imeelezwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu Pinda kupitia Wizara ya Habari na Michezo alitoa 90m kwa Halmashauri ya Igunga ili zikopeshwe kwa vikundi vya vijana. Kingu alikuwa mlezi wa vikundi hivi. Kama mnakumbuka kuna kipindi alianzisha vikundi vikawa maarufu sana vikijihusisha na kilimo cha vitunguu na mpunga. Halmashauri ilipopokea pesa ikaongeza na 5M kama mchango wake ikalipa kwa Vijana SACCOS milioni 95 tarehe 7/10/2013 kupitia vocha 1/9, Cheque No.804 kisha Vijana SACCOS ikakiri kupokea pesa hiyo tarehe 7/10/2013 risiti no.0135. Ikumbukwe kwamba SACCOS hii ilikuwa chini ya usimamizi wa Kingu.

Ripoti inasema kwamba SHS.26,700,000 tu ililipwa kwa vikundi vitano vilivyokusudiwa. SHS.80,800,000 zililipwa kwa vikundi hewa ikiwepo akaunti ya Kingu SHS. 24,000,000 na mfanyabiashara Zengo SHS.15,000,000

Ripoti inaongeza kuwa Elibariki alidanganya mbele ya Waziri Mkuu Pinda, Mkuu wa Mkoa, Naibu waziri wa Michezo na makamera ya TBC kwa kuonyesha shamba la mpunga hewa. Lilionyeshwa shamba la mtu mwingine akidanganya kwamba ni la kikundi.Aidha ripoti inadokeza kuwa mpaka sasa hakuna hata senti iliyorejeshwa kwa kuwa vikundi hivyo pamoja na SACCOS viliyeyuka mara tu baada ya pesa kugawanywa.

2. Mkopo toka halmashauri kwenda kwa DC safari ya China SHS.6,174,585

Ripoti inasema kuwa Mh.DC alikopeshwa SHS.6,174,585 na halamshauri kwa ajili ya safari ya kwenda China kwenye mafunzo 2/8/2014 to 21/8/2014. Hata hivyo CAG anatilia mashaka kuna uwezekano safari hiyo ilikuwa hewa kwani pesa ililipwa 12/1/2015 wakati barua ya mwaliko ilisema ni mafunzo ya 2/8/2014 to 21/8/2014.

Hata hivyo mkopo huo haukuwahi kurejeshwa na bwana huyo. Haaaaa haaaaa huu si usanii wakuu?

PCCB wa Igunga mko wapi jamani, mpaka CAG atoke Dar aje kugundua yote haya na nyie mpo tu……..haya nawamegea huu udondozi toka kwenye Management Letter ya CAG 2014/2015.
 
Halafu huyu Kingi si ndiyo alijifanya hataki hela za sitting allowance bungeni?
 
Back
Top Bottom