VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Nasema kutoka ndani ya chama hiki hiki. Jambo muhimu. Jambo la kidemokrasia. Kwamba, mfumo wa chama kimoja, chama kushika hatamu, ulishafutwa mwaka 1992 na sasa tuna vyama vingi. CCM ndicho chama tawala. Kinatawala kwakuwa kimetoa Rais na kuunda Serikali.
Lakini, vyama vya upinzani navyo vina mafanikio yao. Kwakuwa navyo vilipambana kwenye uchaguzi wa mwaka jana. Navyo vilishinda Ubunge, Udiwani na kadhalika. Lakini, CCM inaonekana kutoridhika. Inataka vyote. Kwa yanayoendelea Zanzibar na Dar-kwenye uchaguzi wa Meya, ni dhahiri kuwa CCM ni mtaka yote.
Kurudiwa uchaguzi Zanzibar ni kubariki ukiukwaji wa Katiba na Sheria za Zanzibar kulikofanywa na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha. Jecha alifuta uchaguzi visivyo. Kama kufuta si halali, kutakuwaje halali kurudiwa kwa uchaguzi. Kutaka yote. Dar es Salaam nako kwazizima. Uchaguzi wa Meya ni kaa la moto.
Ndani ya Dar, Madiwani wa UKAWA ni wengi katika Manispaa za Ilala na Kinondoni na hata jiji lote kwa ujumla. Ndiyo kusema, kimahesabu, UKAWA watatoa Mameya wa Ilala, Kinondoni na hata Meya wa Dar es Salaam. Lakini, CCM inacheza rafu. Inaingiza wapigakura hewa. Wasio Madiwani halali wanaitwa halali. Kutaka yote.
CCM ina Serikali. Zanzibar na Dar es Salaam zina upekee gani hadi kupigwe sarakasi zote hizi? Au mfumo wa chama kimoja urejeshwe? Waziri wa Katiba na Sheria, Mh.Mwakyembe aweza kupeleka Muswada wa Sheria wa Kura ya Maoni juu ya kurejeshwa kwa mfumo wa chama kimoja!
Wazanzibari na Wana-Dar es Salaam waachwe wapate viongozi wanaowataka!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Last edited: