Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Kama kweli mnaamini kuwa Jaji Warioba amewasaliti,mfukuzeni. Kama kweli mnaamini kuwa Jaji Warioba na Tume yake 'wamepika' Rasimu kwa chuki na hila zao na kuacha maoni ya wananchi kama mnavyodai,mfukuzeni chamani mwenu. Kama kweli mnaamini kuwa mnahitaji muda wa kutosha wa kumkashifu,kumtusi,kumsimanga na kumkebehi Jaji Warioba ndani ya chama chenu,Bungeni na kwingineko,mtimueni chamani kwa kumvua uanachama wake.
Mkifanya hivyo itakuwa poa. Mtakuwa na kila nafasi na muda wa kusema mtakayo juu yake. Wafuatiliaji wa siasa za nchi hii mnatuchosha. Tunawaona ni wa ndimi-mbili kuigiza kumponda Jaji Warioba wakati mnaye chamani.Na mnamheshimu kama Kada mkongwe na mtiifu kwa chama. Kama mmeweza kumfukuza Mansoor wa Kiembesamaki hivi karibuni,mnashindwa nini kwa Jaji Warioba.
Kama hamuwezi,mwacheni Jaji Warioba asimamie anachokiamini. Asimamie Maoni ya Wananchi aliyoyakusanya na Tume yake toka sehemu mbalimbali za nchi hii na kuyaainisha katika Rasimu. Msiendelee na kuonyesha mchezo wa kuigiza.