Tafakuri gani ya miaka 50! Tena hata baada ya muda wote huo Mkuu anasema hajui chanzo cha umaskini wetu! Tatizo kuu la CCM, hasa ya miaka hii, ni UONGO, GHILIBA, na PROPAGANDA ZA KIZUSHI; silaha ambazo kwa kweli hazitakifikisha chama mahali popote tena kwa hasara ya taifa.
Laiti CCM ingeukubali ukweli kama ulivyo na kuchukua hatua lakini hili ndani ya chama hiki, kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ni vigumu kufikiwa angalau kwa kizazi hiki. Hata hivyo, uzuri ni kwamba kushindana na UKWELI ni kama kupiga ngumi ukutani.