CCM Mbeya mnatia aibu!

gwa myetu

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
4,473
4,665
Nimezunguka wilaya na mikoa mingi Tanzania bara , kote huko nimeona ccm ikiwa na vitrga uchumi vya kutosha kubwa zaidi ni osifi zenye hadhi kubwa maghorofa Kwa maghorofa lakini hii ni tofauti na Mbeya yaani ofisi yao ya chama kama choo cha stand au mabanda ya kuku , yaani ofisi zimejipanga hovyo hovyo kama madarasa ya shule ya msingi .

CCM makao makuu kumbukeni Mbeya mna wapiga kura wengi sana na ni ngome muhimu ya ccm hivyo wakumbekeni Kwa kuwajengea jengo la ofisi za mkoa angalau hata ghorofa moja kama la pale wilayani Mafinga angalau maana tukisema mjenge kama la Arusha , Dodoma au Tanga ndo hadi Nyerere afufuke!! Yaani wamebaki kujivunia uwanja wa sokoine ambao hauna hata hadhi ya uwanja wa Karume pale TFF
 
Back
Top Bottom