Ccm leo ndani ya kata ya nkoanrua alikozaliwa edo lowassa

luvcyna

JF-Expert Member
Feb 24, 2009
1,848
1,938
salam sana wanajamii wenzangu... Napenda kuwaletea taarifa kuwa CCM ndo wamepania kufunika haswa katika kata mama wanayoitegemea kuliko zote kata ya Nkoanrua ambayo katika uchaguzi uliopita ilimbeba mgombea wao Jeremia Sumari vilivyo na kumuachia nassary kura 28. Baada ya CDM kupita maeneo hayo siku ya alhamisi na kufanya mageuzi makubwa ya kifikra na kujaza umati wa ajabu kiasi cha kutoenea uwanja wa shule ya msingi Nkoanrua leo ni muda muafaka kupima muitikio wa wananchi wa kata hii kwa kile walicholishwa Alhamisi na mheshimiwa Dr. W.P.Slaa kama kimekuwa digested ama vomited.

Katika kuonyesha kuwa wamepania vilivyo kuwahadaa wakazi wa eneo hili, CCM wamekuja na wasanii lukuki kama Khadija Kopa, Diamond,Origino Komedy, na vikundi kadhaa vya sanaa. Naye Nchema anasubiriwa vilivyo kujibu tuhuma alizorushiwa katika mkutano wa CDM uliopita.

Nawasilisha natafuta picha kwa hudi na uvumba...mwenye taarifa zaidi ya nilizo nazo tafadhali funguka
 
napata taarifa kuwa wananchi wa eneo hili kotokana na kutopata fursa ya kuuliza maswali katika mikutano mingi ifanywayo na vyama vya siasa wameandaa maswali yao kimaandishi ambapo yatakabidhiwa na muwakilishi wao pindi Siyoi apandapo jukwaani kujibu tuhuma mbalimbali, ikumbukwe kuwa hili ndilo eneo hasa lililoathirika mno na bomoa bomoa ya kupisha ujenzi wa kupanua barabara ya kufikirika tangu 2006 hadi leo ambapo mabadiliko yalioko kwenye barabara hiyo ni wingi wa mashimo na mifereji katikati ya barabara hiyo
 
Back
Top Bottom