CCM la kuvunda halina ubani

CCM la kuvunda halina ubani

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,744
Reaction score
2,615
Ni wazi kwamba Chama cha Mapinduzi kina la kujibu kuhusu hoja alizotoa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole na hasa suala la lkumpitisha mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia Suuluhu Hassan.

Katika barua yake aliyotangaza kujiuzuku Julai 13 na baadaye mkutano wake na waandishi wa habari wa Julai 18, Polepole ameeleza kinagaubaga namna (kwa maoni yake) utarataibu wa kumpitisha mgombea ulivyokiuka katika mkutano mkuu uliofanyika Januari 19, 2025 jijini Dodoma.

Miongoni mwa mambo aliyoibua ni utaratibu wa CCM kupokea majina yasiyopungua matatu ya wagombea na kisha wagombea hao kujadiliwa na mkutano mkuu, jambo ambalo halikufanyika.

Katika mkutano ule, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alishauri mgombea huyo ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa mkutabo mkuu, atoke nje ili wamjadili, lakini Rais Samia alikataa akiwataka wajumbe wajadili mambo yote kwa uwazi. Hilo ndilo linalokosolewa, kwamba utaratibu ulikiukwa.

Alichokielea Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa wajumbe:

Polepole ametoa mfano wa mkutano mkuu wa 2020, ambao aliyekuwa mwenyekiti wa mkutabo, Hayati Rais John Magufuli alitoka nje na kumwachia Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aongoze kikao.

Sasa, kwa nini Rais Samia hakutoka nje? Alikuwa anaogopa wajumbe kumkataa?

Mchambuzi wa masuala ya siasa Dk Dennis Muchunguzi amefafanua:

Japo wapo wanaosema kuwa suala la mgombea mmoja kwa marais wanaoingia kipindi cha pili ni utamaduni wa CCM, lakini utamaduni huo haupaswi kukandamza demokrasia. Hata kama kama wakati wa Rais Magufuli, Marehemu Bernard Membe alifukuzwa uanachama kwa kuonyesha nia ya kugombea, ndio kosa lirudiwe kwa kosa?

Tulishuhudia kabla ya Rais Samia kupitishwa kuwa mgombea, kukiwa na kampeni ya utoaji wa fomu moja ya urais. Viongozi mbali wa CCM na Serikali walikuwa wakimpigia kampeni waziwazi wakisema fomu ya urais ni moja.

Haikuishia hapo, wakaenda mbali na kuanza kumchangia ada ya kuchukua fomu hiyo, makundi kwa makundi yakawa yakichanga fedha kwa ajili ya fomu ya urais. Huko kote ilikuwa ni kukandamiza demokrasia ndani ya CCM.

Pengine ifike mahali sasa CCM iweke wazi kwamba Rais aliyeko madarakani anaweza kupingwa na makada wengine au asipingwe, ili kuondoa hisia za kumhujumu rais. Vinginevyo hakutakuwa na maana kama chama kinajitangaza kuwa cha kidemokrasia lakini kinazuia makada wengine kugombea.

Alichokisema Polepole, kilisemwa pia na kada wa chama hicho, Mchungaji Godfrey Malisa, lakini uongozi wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro ulimfutia uanachama wake. Hiyo ilifanyika ilikuzima uvundo uliofanyika kwenye kutano mkuu.

Lakini Waswahili wanasema, la kuvunda halina ubani. Polepole naye amekuja kufukua uvundo. Inawezekana CCM wakaendelea kuziba masikio na kufunika, lakini harufu ya malalamiko ya wanachama itaendelea hata baada ya uchaguzi. Kuna hatari ya kuwa na viongozi waliochaguliwa lakini wamekosa uhalali mbele ya macho ya wananchi.
 
Hii imekaa vizuri sana hii, hivi na Kikwete wakati wake alitoka nje au aligoma kutoka nje? Dawa ya Kiburi ni Jeuri
 
Out of topic -- wameanza kuhujumu Facebook muda huu.
 
Ni kweli, kitu kilichooza hata umwage ubani wa toka uarabuni hamna kitu yaani kitu kinatemaa balaa.
 
1753103858021.png
1753103858021.png
1753103858021.png

Ni wazi kwamba Chama cha Mapinduzi kina la kujibu kuhusu hoja alizotoa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole na hasa suala la lkumpitisha mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia Suuluhu Hassan.

Katika barua yake aliyotangaza kujiuzuku Julai 13 na baadaye mkutano wake na waandishi wa habari wa Julai 18, Polepole ameeleza kinagaubaga namna (kwa maoni yake) utarataibu wa kumpitisha mgombea ulivyokiuka katika mkutano mkuu uliofanyika Januari 19, 2025 jijini Dodoma.

Miongoni mwa mambo aliyoibua ni utaratibu wa CCM kupokea majina yasiyopungua matatu ya wagombea na kisha wagombea hao kujadiliwa na mkutano mkuu, jambo ambalo halikufanyika.

Katika mkutano ule, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alishauri mgombea huyo ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa mkutabo mkuu, atoke nje ili wamjadili, lakini Rais Samia alikataa akiwataka wajumbe wajadili mambo yote kwa uwazi. Hilo ndilo linalokosolewa, kwamba utaratibu ulikiukwa.

View attachment 3413156

Alichokielea Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa wajumbe:

View attachment 3413159

Polepole ametoa mfano wa mkutano mkuu wa 2020, ambao aliyekuwa mwenyekiti wa mkutabo, Hayati Rais John Magufuli alitoka nje na kumwachia Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aongoze kikao.

View attachment 3413160
Sasa, kwa nini Rais Samia hakutoka nje? Alikuwa anaogopa wajumbe kumkataa?

Mchambuzi wa masuala ya siasa Dk Dennis Muchunguzi amefafanua:

View attachment 3413161

Back
Top Bottom