CCM kutokemea kuzomewa kwa Rais mstahafu wa ZNZ ni kuunga mkono au kughafilika?

dapam

Senior Member
Dec 19, 2014
108
37
Jana kwenye sherehe za kutimia miaka 52 ya mapinduzi ya zanzibar tumeshuhudia kitendo cha aibu kilichofanywa na wanaccm wa Zanzibar cha kumzomea Rais mstahafu wa awamu ya sita wa Serekali ya mapinduzi ya Zanzibar mh. Amaan Abeid Amaan Karume.
Kitendo hicho sio tu kimeifedhehesha CCM bali kimewaonyesha Watanzania kwamba kuna tatizo kumbwa ndani ya CCM Zanzibar.
Cha kusikitisha ama kushangazza ni kitendo cha viongozi wa CCM Zanzibar kulikalia kimya jambo hili je ni kutuaminisha kwamba wanakiunga mkono kitendo kile au wameghafilika kukikemea?
 
Sio kuzomea tu bali huku Tanganyika alipigwa vibao na alizomewaga Waziri mkuu mstaafu Mzee Warioba, Mwenyekiti wao akasifia na Kusema eti Mzee Warioba "alijitakia mwenyewe!
 
Ewe Mola wetu,muumba wa ardhi na mbingu na vyote vilivyomo ndani yake,tunapiga magoti na kunyanyua mikono yetu juu kukuomba wewe Mtukufu,mwenye kila uwezo kutujaalia amani na usalama katika nchi yetu....Aaaaamin
 
CCM vipande-vipande Zanzibar.
Tanzania bara ilikuwa hivyo baada ya CCM kumegwa na akina Lowasa na wapiga filimbi wa hamelini wao akina Kingunge,na sumaye kilichowakuta hao CCM Lowasa unakijua ndicho hicho hicho kitawakuta hao wagawa CCM wa ZANZIBAR.SOMO LA KUJIFUNZA WANALO LA BARA.Mwenye macho haambiwi tazama.CCM ina uzoefu wa kupambana na wagawa CHAMA .
 
Halafu wemegeuza Public holiday kuwa ni sherehe za kichama..ndiyo maana hata hiyo zomeazomea inatokea kwa kudhan wapo kwenye maadhimisho ya CCM
 
ami jei hawajielewiiiiiiiiiiiiii
Afrika moto...akina Nkurunziza kila mahali, kuanzia Zanzibar nchi aliyopigania John Okelo hadi katika nchi yake ya asili Uganda unakutana na Mseveni...anasema aliipigania nchi anayetaka kumtoa naye aende msituni...vuka kwa Kagame hadi 2034 kisha Nkurunziza hatujui hadi lini...dogo letu Kabila nalo mambo yale yale kama bado anasafiri na mabasi ya Msae hapa Tz....tuna nini waafrika na madaraka???? Nahisi tuna wenda wazimu
 
j
Tanzania bara ilikuwa hivyo baada ya CCM kumegwa na akina Lowasa na wapiga filimbi wa hamelini wao akina Kingunge,na sumaye kilichowakuta hao CCM Lowasa unakijua ndicho hicho hicho kitawakuta hao wagawa CCM wa ZANZIBAR.SOMO LA KUJIFUNZA WANALO LA BARA.Mwenye macho haambiwi tazama.CCM ina uzoefu wa kupambana na wagawa CHAMA .
Zanzibar sio bara .Just wait and see mr. Hamelin
 
Tanzania bara ilikuwa hivyo baada ya CCM kumegwa na akina Lowasa na wapiga filimbi wa hamelini wao akina Kingunge,na sumaye kilichowakuta hao CCM Lowasa unakijua ndicho hicho hicho kitawakuta hao wagawa CCM wa ZANZIBAR.SOMO LA KUJIFUNZA WANALO LA BARA.Mwenye macho haambiwi tazama.CCM ina uzoefu wa kupambana na wagawa CHAMA .
Yehoda,
Unatoa majibu mepesi sana kwenye tatizo linalotakiwa kuwa analyzed na kutolewa majibu ya kina na suluhu. Kumbuka kuwa hizi nchi (Tanganyika na Zanzibar) si za mtu wala kikundi cha watu na pia si mali ya CCM! Mtu anapokuja na mawazo tofauti na ya kwenu/ kwako asionekani haitakii mema nchi yake!
Suala la kumzomea mstaafu ni kitendo cha kihuni na kinatakiwa kulaaniwa tena hadharani! Kwani hao wanaokitetea kitendo hicho wanauhakika gani kama nao hawatazomewa siku moja kama hili halikemewi?
 
Back
Top Bottom