Hodi hapa barazani, salaam!
Hoja ya haja,
Kwakua wakati wa uteuzi wa spika walitumia kigezo cha jinsia ili kuwaengua baadhi ya watu (Samuel Sitta mathalani) kutoka kwenye kinyanganyiro cha uspika, je kigezo hicho hicho kinaweza kutumika mwaka 2015 kuteua mgombea mwanamke kwenye Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM. Hii inatokana na ukweli kwamba mvutano unaweza kuwa mkubwa kiasi cha kutishia mgawanyiko wa chama.
Naomba kuwasilisha.
NB: hii ni post yangu ya kwanza hapa jamvini nipo tayari kukosolewa kama hoja itaonekana kuwa na uzito wa unyoya.

kama cdm wataendelea na spidi hii hii hakuna mgombea mwanamke kutoka ccm atakayefua dafu mbele ya mgombea kutoka cdm

Wacha uongo wewe kwanini asishinde? acha kuendekeza mfumo dume, mwanamke na mwanamume wanafanana kiutendaji kwani urais unahitaji akili au msuli? isitoshe CCM hata wakimsimamisha Anna Makinda anaweza kupita kwa kishindo itategemeana na utashi wa akina Lewis Makame na kundi lake lililowekwa na Chama pale kutekeleza maagizo ya chama. Ndiyo maana inatakiwa mimi na wewe tukeshe tukiomba dua katiba yetu ibadilishwe au tupate Tume huru ya uchaguzi ili kwa mara ya kwanza tushuhudie uchaguzi nchini kwetu.
Piga ua, mafisadi nguvu zao za pesa watazipeleka kwa chaguo lao ambaye ni Sophia Simba achukue Urais kilaini huku akiwacha akina Dr. Slaa, Peter Mziray, Husein Rungwe na Dovutwa kwa mbali!