CCM kusifia kila kitu kunawasaidia nini?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,300
33,919
CCM wana tabia ya kusifia kila kitu kinachofanywa na viongozi wao hadi inafika wakati inashangaza sana. CCM huwa haina uelekeo zaidi ya ule anaokuwa nao Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho kwa wakati husika.

Enzi za Mwalimu akiwa Mwenyekiti wa chama chao ulikuwa unaweza kudhani kwamba kila mtu ndani ya CCM ni Mjamaa kweli kweli hadi wengine wakawa wanaitana "Komredi". Mwalimu alipong'atuka akaenda na CCM yake ya aina hiyo.

Alipoingia Mwinyi alikuja na sera ya kufungua milango na kuleta sera ya kuhalalisha sekta binafsi. Hapo wana CCM wakajitwisha kazi ya kutetea ni kwa nini Azimio la Arusha lilizikwa kule Zanzibar. Kila mwana CCM akawa anapigana kuonesha njia sahihi ni kutoka kwenye Ujamaa na kwenda kwenye ubepari Uchwara.

Alipoingia Mkapa yeye aliendeleza yaliyoanzishwa na Mwinyi ila yeye akaongeza na Mbwembwe za kusema mambo yake atayafanya kwa "uwazi na Ukweli". Mkapa ndiye aliyeibeba sera ya ubinafsishaji kwa mbwembwe nyingi sana na wakati mwingine kwa kutumia nguvu za dola (Rejea: Net Group Solution).

Kikwete alipokuja na kauli mbiu yake ya "Ari Mpya. Kasi Mpya na Nguvu Mpya" wana CCM walipagawa nae mpaka ikaonekana kama ni mkombozi toka mbinguni kaja kuwakomboa watanzania. Yaliyotokea ni Historia.

Leo CCM ina mwenyekiti Mpya mwenye harakati za kuijenga "CCM Mpya". Sasa kila mwana CCM anaongea ni kama vile wenyeviti wote wa chama hicho waliopita hawana sifa za kufanana hata kidogo na Mwenyekiti wao wa sasa John Pombe Magufuli.

Kwa ivo kwa wana CCM akili huja pale tu unapokuwa Kiongozi ndani ya chama hicho. Inavoelekea ni kama vile wana CCM wanataka kuonesha kwamba mtu akiwa kiongozi ndani ya chama hicho "anatukuka" na kuwa na akili "zisizo za kawaida".

Mambo yaliyoifikisha Tanzania hapa ilipo yote yalifanywa na Viongozi wa CCM na wakati wakiyafanya wana CCM waliwasifia sana na wale waliowapinga walionekana sio wazalendo.

Swali la kujiuliza hivi wana CCM hupata faida gani kwa kusifia kila linalofanywa na viongozi wao hata kama ni baya dhidi ya mustakabali wa Taifa letu la Tanzania?
 
Back
Top Bottom