CCM kumruhusu Lusinde atukane mmejiponza na kuruhusu "shujaa" aoge kashfa bila huruma

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,798
71,218
Kama kawaida ya CCM kutokutumia akili inapofika masuala ya kujibu hoja zilizoibuliwa bali kumtumia mbunge wa Mtera Lusinde au wa Geita Musukuma ambao hawana elimu ya kuelewa wanapaswa kusema nini kwa wakati gani, wamefungulia mjadala zaidi dhidi ya matendo ya hovyo yaliyotendwa na Magufuli na watu wake katika awamu ya tano.

CCM inadhani Lusinde kumshambulia Mbowe na Chadema bungeni huku akishangiliwa na wabunge wa CCM wakiongozwa na PM Majaliwa (ambaye leo amejionyesha kuwa he is too low for the post) basi jamii ya kitanzania itawaona wanawatetea kumbe inaongeza gap lililopo na hasira kwao.

Maumivu ya Mbowe kuhusu TRA mtu akiyabeza ajue anajenga hasira na kundi kubwa la wafanyabiashara na watumishi wao pia familia zao ambazo zimeyaona machungu ya aina hiyo.

SASA WAKAE MKAO WA KILIO KWANI MASHAMBULIZI DHIDI YA HUYO WANAYEMTETEA NDIO WAMEYAIDHINISHA RASMI WENYEWE.

Mwenda zake na vibaraka wake waliobaki duniani mbona watashangaa!
 
Mbowe kabla hata ya kujisafisha na uongo wake wa kulewa na kuangushwa na konyagi kisha kulitangazia taifa kwamba amepigwa na wasiojulikana, amekuja na igizo jingine kwamba alifilisiwa na akaunti zake zote zilifungwa na TRA!!

Kama ni kweli alikuwa wapi kuyasema haya? Badala yake akawa anaitisha press conference akiwa amevaa gloves feki huku akiwa amejifungia kwenye lockdown hewa.

Ina maana Mbowe alikuwa tayari kuita waandishi wa habari na kuwaelezea alivyokimbia bunge na kwenda lockdown uchwara kuliko kuwaelezea alivyofungiwa akaunti zake zote ikiwemo ya mshahara?

Mbowe hili ni taifa la watu wanaojitambua na kamwe hutafanikiwa kwenye hiyo biashara yako mpya uliyokula 10% ili ulete chanjo ya corona nchini.
 
Hatukatai kuwa Mbowe kalidanganya Taifa, Lakini kama kadanganya tafsiri rahisi ni kwamba ameizushia kashfa na kuichafua Mamlaka ya Mapato (TRA). Kwa Mujibu wa sheria hili ni kosa, kama ni kosa iko wapi TRA Leo ijitokeze hadharani kumkemea na pengine kumfungulia mashitaka Mbowe?? Uhalisia wa awamu ya tano unafahamika na kila mtu, msitumie nguvu nyingi kuwageuza Watanzania wajinga!!
 
Back
Top Bottom