Kumbukeni wiki kadhaa zilizopita Uhuru Kenyatta na Ruto walifika Ikulu ya DAR na kuteta na JK. Vyombo vya habari viliripoti kiduchu. Lakini binafsi naamini walikuwa wanatafuta support ya TZ. Sasa Raila aliona si vizuri kutumia JK ila yeye apitie kwa MAGUFULI pengine si kwa sababu ya urafiki tu lakini vilevile jamaa aliona pengine Dkt. Magufuli anaheshimika hapa TZ, hivyo, akienda KENYA anawezabadilisha upepo wa siasa. Wakati huo huo, DKt. Magufuli alipaswa kumpa msimamo wake kuwa anakwenda lakini inaweza kutoa picha tofauti kwa serikali mbili hizo, kwamba CCM inamtaka RAILA na si wengine, na hapa ndipo alipaswa kutumia busara na si umaarufu! Hata hivyo, hakuomba ruhusa toka kwa MKUU wake wa kazi? Alieleza anakwenda kufanya nini? Je, Wakenya watapata picha gani kwa JK na CCM yake? Hapo hamna urafiki.